Exodus 6:27 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Ndio haohao Mose na Aroni walioongea na Farao, mfalme wa Misri, juu ya kuwatoa Waisraeli nchini Misri.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Hao ndio waliozungumza na Farao, mfalme wa Misri kuhusu kuwatoa Waisraeli Misri. Ilikuwa ni huyo Musa na huyo Haruni.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Ni hao walionena na Farao mfalme wa Misri ili wawatoe wana wa Israeli watoke Misri; hao ni Musa ye yule, na Haruni ye yule.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Ndio haohao Mose na Aroni walioongea na Farao, mfalme wa Misri, juu ya kuwatoa Waisraeli nchini Misri.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Ndio hao hao waliozungumza na Farao mfalme wa Misri kuhusu kuwatoa Waisraeli Misri. Ilikuwa ni huyo Mose na huyo Aroni.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Ndio hao hao waliozungumza na Farao mfalme wa Misri kuhusu kuwatoa Waisraeli Misri. Ilikuwa ni huyo Musa na huyo Haruni.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Ni hao walionena na Farao mfalme wa Misri ili wawatoe wana wa Israeli watoke Misri; hao ni wale wale Musa na Haruni.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Ndio haohao Mose na Aroni walioongea na Farao, mfalme wa Misri, juu ya kuwatoa Waisraeli nchini Misri.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Wao ndio waliosema na Farao, mfalme wa Misri, wapate kuwatoa wana wa Isiraeli huko Misri, yeye Mose naye Haroni.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Ni hao walionena na Farao mfalme wa Misri ili wawatoe wana wa Israeli watoke Misri; hao ni Musa ye yule, na Haruni ye yule.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Ndio haohao Musa na Haruni walioongea na mufalme wa Misri, juu ya kuwatoa Waisraeli kutoka inchi ya Misri.