Exodus 6:8 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Nami nitawapeleka katika nchi ile niliyoapa kumpa Abrahamu, Isaka na Yakobo. Nitawapeni nchi hiyo iwe yenu. Mimi ni Mwenyezi-Mungu.’”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Nami nitawaleta hadi nchi niliyoapa kwa mkono ulioinuliwa kumpa Ibrahimu, Isaka na Yakobo. Nitawapa iwe milki yenu. Mimi ndimi Mwenyezi Mungu.’ ”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Nami nitawaleta hata nchi ile ambayo naliinua mkono wangu, niwape Ibrahimu, na Isaka, na Yakobo; nitawapa iwe urithi wenu; Mimi ni YEHOVA.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Nami nitawapeleka katika nchi ile niliyoapa kumpa Abrahamu, Isaka na Yakobo. Nitawapeni nchi hiyo iwe yenu. Mimi ni Mwenyezi-Mungu.’”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Nami nitawaleta mpaka nchi niliyoapa kwa mkono ulioinuliwa kumpa Abrahamu, Isaki na Yakobo. Nitawapa iwe milki yenu. Mimi ndimi BWANA.’ ”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Nami nitawaleta mpaka nchi niliyoapa kwa mkono ulioinuliwa kumpa Ibrahimu, Isaka na Yakobo. Nitawapa iwe milki yenu. Mimi ndimi bwana.’ ”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Nami nitawaleta hata nchi ile ambayo niliinua mkono wangu, niwape Abrahamu, na Isaka, na Yakobo; nitawapa iwe urithi wenu; Mimi ni YEHOVA.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Nami nitawapeleka katika nchi ile niliyoapa kumpa Abrahamu, Isaka na Yakobo. Nitawapeni nchi hiyo iwe yenu. Mimi ni Mwenyezi-Mungu.’”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Nami nitawapeleka katika hiyo nchi, niliyoiapia na kuuinua mkono wangu kwamba: Nitampa Aburahamu na Isaka na Yakobo; hiyo ndiyo, mimi Bwana nitakayowapa ninyi, iwe yenu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Nami nitawaleta hata nchi ile ambayo naliinua mkono wangu, niwape Ibrahimu, na Isaka, na Yakobo; nitawapa iwe urithi wenu; Mimi ni YEHOVA.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Nami nitawapeleka katika inchi ile niliyoapa kumupa Abrahamu, Isaka, na Yakobo. Nitawapa inchi hiyo ikuwe yenu. Mimi ni Yawe.’ ”