Exodus 7:10 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Basi, Mose na Aroni wakamwendea Farao na kufanya kama walivyoamriwa na Mwenyezi-Mungu. Aroni aliitupa fimbo yake chini mbele ya Farao na maofisa wake, nayo ikawa nyoka.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Ndipo Musa na Haruni wakaenda kwa Farao, wakafanya sawasawa na jinsi Mwenyezi Mungu alivyoagiza. Haruni akaitupa ile fimbo yake chini mbele ya Farao na maafisa wake, nayo ikawa nyoka.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Basi Musa na Haruni wakaingia kwa Farao, wakafanya vivyo kama Bwana alivyowaambia; Haruni akaibwaga fimbo yake chini mbele ya Farao, mbele ya watumishi wake, ikawa nyoka.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Basi, Mose na Aroni wakamwendea Farao na kufanya kama walivyoamriwa na Mwenyezi-Mungu. Aroni aliitupa fimbo yake chini mbele ya Farao na maofisa wake, nayo ikawa nyoka.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Ndipo Mose na Aroni wakaenda kwa Farao wakafanya sawasawa kama vile BWANA alivyoagiza. Aroni akaitupa ile fimbo yake chini mbele ya Farao na maafisa wake, nayo ikawa nyoka.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Ndipo Musa na Haruni wakaenda kwa Farao wakafanya sawasawa kama vile bwana alivyoagiza. Haruni akaitupa ile fimbo yake chini mbele ya Farao na maafisa wake, nayo ikawa nyoka.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Basi Musa na Haruni wakaingia kwa Farao, wakafanya vivyo hivyo kama BWANA alivyowaambia; Haruni akaibwaga fimbo yake chini mbele ya Farao, mbele ya watumishi wake, ikawa nyoka.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Basi, Mose na Aroni wakamwendea Farao na kufanya kama walivyoamriwa na Mwenyezi-Mungu. Aroni aliitupa fimbo yake chini mbele ya Farao na maofisa wake, nayo ikawa nyoka.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Mose na Haroni walipofika kwake Farao wakafanya hivyo, kama Bwana alivyowaagiza: Haroni alipoitupa fimbo yake chini mbele yake Farao na mbele yao watumishi wake, ikawa nyoka.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Basi Musa na Haruni wakaingia kwa Farao, wakafanya vivyo kama BWANA alivyowaambia; Haruni akaibwaga fimbo yake chini mbele ya Farao, mbele ya watumishi wake, ikawa nyoka.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Basi, Musa na Haruni wakamwendea mufalme wa Misri na kufanya kama vile walivyoamuriwa na Yawe. Haruni akatupa fimbo yake chini mbele ya mufalme na wakubwa wake, nayo ikakuwa nyoka.