Exodus 7:11 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Lakini, Farao akawaita wenye hekima wake na wachawi; hao wachawi wa Misri wakafanya vivyo hivyo kwa uchawi wao.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Farao naye akawaita watu wenye maarifa na wachawi na waganga wa Misri, nao wakafanya vivyo hivyo kwa siri ya uganga wao.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Ndipo Farao naye akawaita wenye akili na wachawi; na hao waganga wa Misri wakafanya vivyo kwa uganga wao.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Lakini, Farao akawaita wenye hekima wake na wachawi; hao wachawi wa Misri wakafanya vivyo hivyo kwa uchawi wao.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Farao naye akawaita watu wenye maarifa na wachawi na waganga wa Kimisri, nao wakafanya vivyo hivyo kwa siri ya uganga wao.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Farao naye akawaita watu wenye maarifa na wachawi na waganga wa Kimisri, nao wakafanya vivyo hivyo kwa siri ya uganga wao.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Ndipo Farao naye akawaita wajuzi na wachawi; na hao waganga wa Misri wakafanya vivyo hivyo kwa uganga wao.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Lakini, Farao akawaita wenye hekima wake na wachawi; hao wachawi wa Misri wakafanya vivyo hivyo kwa uchawi wao.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ndipo, Farao naye alipowaita wajuzi na walozi, nao hao waganga wakafanya hivyo kwa uganga wao.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Ndipo Farao naye akawaita wenye akili na wachawi; na hao waganga wa Misri wakafanya vivyo kwa uganga wao.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Lakini, mufalme wa Misri akawaita wenye hekima wake na wachawi. Wale wachawi wa Misri wakafanya vile vile kwa uchawi wao.