Exodus 7:20 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mose na Aroni wakafanya kama Mwenyezi-Mungu alivyowaamuru. Aroni aliinua fimbo yake juu mbele ya Farao na maofisa wake, akayapiga maji ya mto Nili, na maji yote mtoni yakageuka kuwa damu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Musa na Haruni wakafanya kama vile Mwenyezi Mungu alivyokuwa amewaagiza. Akainua fimbo yake machoni pa Farao na maafisa wake na kuyapiga maji ya Mto Naili, na maji yote yakabadilika kuwa damu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Musa na Haruni wakafanya hivyo, kama Bwana alivyowaambia; naye akaiinua ile fimbo, na kuyapiga maji yaliyokuwa mtoni, mbele ya Farao, mbele ya watumishi wake; na hayo maji yote yaliyokuwa katika mto yakageuzwa kuwa damu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mose na Aroni wakafanya kama Mwenyezi-Mungu alivyowaamuru. Aroni aliinua fimbo yake juu mbele ya Farao na maofisa wake, akayapiga maji ya mto Nili, na maji yote mtoni yakageuka kuwa damu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Mose na Aroni wakafanya kama vile BWANA alivyokuwa amewaagiza. Akainua fimbo yake machoni pa Farao na maafisa wake na kuyapiga maji ya Mto Nile, na maji yote yakabadilika kuwa damu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Musa na Haruni wakafanya kama vile bwana alivyokuwa amewaagiza. Akainua fimbo yake machoni pa Farao na maafisa wake na kuyapiga maji ya Mto Naili, na maji yote yakabadilika kuwa damu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Musa na Haruni wakafanya hivyo, kama BWANA alivyowaambia; naye akaiinua ile fimbo, na kuyapiga maji yaliyokuwa mtoni, mbele ya Farao, mbele ya watumishi wake; na hayo maji yote yaliyokuwa katika mto yakageuzwa kuwa damu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mose na Aroni wakafanya kama Mwenyezi-Mungu alivyowaamuru. Aroni aliinua fimbo yake juu mbele ya Farao na maofisa wake, akayapiga maji ya mto Nili, na maji yote mtoni yakageuka kuwa damu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Mose na Haroni wakafanya hivyo, kama Bwana alivyoagiza. Haroni alipoinyanyua hiyo fimbo na kuyapiga maji yaliyomo humo mtoni machoni pake Farao napo machoni pao watumishi wake, ndipo, maji yote yaliyomo humo mtoni yalipogeuzwa kuwa damu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Musa na Haruni wakafanya hivyo, kama BWANA alivyowaambia; naye akaiinua ile fimbo, na kuyapiga maji yaliyokuwa mtoni, mbele ya Farao, mbele ya watumishi wake; na hayo maji yote yaliyokuwa katika mto yakageuzwa kuwa damu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Musa na Haruni wakafanya kama vile Yawe alivyowaamuru. Haruni akainua fimbo yake juu mbele ya mufalme wa Misri na wakubwa wake, akayapiga maji ya muto Nili, na maji yote katika muto yakageuka kuwa damu.