Exodus 8:13 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mwenyezi-Mungu akafanya kama Mose alivyomwomba: Vyura wakafa majumbani, viwanjani na kwenye kumbi za nyumba na katika mashamba.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Naye Mwenyezi Mungu akafanya lile Musa alilomwomba. Vyura wakafia ndani ya nyumba, viwanjani na mashambani.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Bwana akafanya sawasawa na neno la Musa; na hao vyura wakafa kutoka katika zile nyumba, na katika viwanja, na katika mashamba.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mwenyezi-Mungu akafanya kama Mose alivyomwomba: vyura wakafa majumbani, viwanjani na kwenye kumbi za nyumba na katika mashamba.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Naye BWANA akafanya lile Mose alilomwomba. Vyura wafia ndani ya nyumba, viwanjani na mashambani.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Naye bwana akafanya lile Musa alilomwomba. Vyura wakafia ndani ya nyumba, viwanjani na mashambani.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
BWANA akafanya sawasawa na neno la Musa; na hao vyura wakafa kutoka katika zile nyumba, na katika viwanja, na katika mashamba.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mwenyezi-Mungu akafanya kama Mose alivyomwomba: Vyura wakafa majumbani, viwanjani na kwenye kumbi za nyumba na katika mashamba.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Bwana akafanya, kama Mose alivyosema: vyura wakafa manyumbani na nyuani na mashambani,
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
BWANA akafanya sawasawa na neno la Musa; na hao vyura wakafa kutoka katika zile nyumba, na katika viwanja, na katika mashamba.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Musa na Haruni wakafanya hivyo. Haruni akainua fimbo yake na kupiga mavumbi, nayo yakageuka kuwa chawa nao wakakuwa juu ya watu na nyama. Mavumbi yote katika inchi yote ya Misri yakageuka kuwa chawa.