Exodus 8:15 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Lakini Farao alipoona kwamba nchi imepata nafuu, akawa mkaidi tena, wala hakuwasikiliza Mose na Aroni, kama Mwenyezi-Mungu alivyokuwa amesema.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Lakini Farao alipoona pametokea nafuu, akaushupaza moyo wake na hakuwasikiliza Musa na Haruni, kama vile Mwenyezi Mungu alivyokuwa amesema.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Lakini Farao alipoona ya kuwa pana nafuu, akaufanya moyo wake kuwa mzito, asiwasikize; kama Bwana alivyonena.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Lakini Farao alipoona kwamba nchi imepata nafuu, akawa mkaidi tena, wala hakuwasikiliza Mose na Aroni, kama Mwenyezi-Mungu alivyokuwa amesema.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Lakini Farao alipoona pametokea nafuu, akaushupaza moyo wake na hakuwasikiliza Mose na Aroni, kama vile BWANA alivyokuwa amesema.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Lakini Farao alipoona pametokea nafuu, akaushupaza moyo wake na hakuwasikiliza Musa na Haruni, kama vile bwana alivyokuwa amesema.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Lakini Farao alipoona ya kuwa pana nafuu, akaufanya moyo wake kuwa mzito, asiwasikize; kama BWANA alivyonena.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Lakini Farao alipoona kwamba nchi imepata nafuu, akawa mkaidi tena, wala hakuwasikiliza Mose na Aroni, kama Mwenyezi-Mungu alivyokuwa amesema.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Lakini Farao alipoona, ya kuwa jambo limetulia, akaushupaza moyo wake, asiwasikie, kama Bwana alivyosema.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Lakini Farao alipoona ya kuwa pana nafuu, akaufanya moyo wake kuwa mzito, asiwasikize; kama BWANA alivyonena.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Wale wachawi wakamwambia mufalme wa Misri: “Hii ni kazi ya mukono wa Mungu.” Lakini moyo wa mufalme ukaendelea kuwa mugumu, wala hakuwasikiliza Musa na Haruni. Ikakuwa kama vile Yawe alivyokuwa amesema.