Exodus 8:19 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Wale wachawi wakamwambia Farao, “Hii ni kazi ya mkono wa Mungu.” Lakini moyo wa Farao ukaendelea kuwa mgumu; wala hakuwasikiliza Mose na Aroni. Ikawa kama Mwenyezi-Mungu alivyokuwa amesema.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Waganga wale wakamwambia Farao, “Hiki ni kidole cha Mungu.” Lakini moyo wa Farao ukawa mgumu naye hakuwasikiliza, kama vile Mwenyezi Mungu alivyokuwa amesema.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Ndipo wale waganga wakamwambia Farao, Jambo hili ni chanda cha Mungu; na moyo wake Farao ukawa mgumu asiwasikize; vile vile kama Bwana alivyonena.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Wale wachawi wakamwambia Farao, “Hii ni kazi ya mkono wa Mungu.” Lakini moyo wa Farao ukaendelea kuwa mgumu; wala hakuwasikiliza Mose na Aroni. Ikawa kama Mwenyezi-Mungu alivyokuwa amesema.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Waganga wale wakamwambia Farao, “Hiki ni kidole cha Mungu.” Lakini moyo wa Farao ukawa mgumu naye hakuwasikiliza, kama vile BWANA alivyosema.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Waganga wale wakamwambia Farao, “Hiki ni kidole cha Mungu.” Lakini moyo wa Farao ukawa mgumu naye hakuwasikiliza, kama vile bwana alivyosema.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Ndipo wale waganga wakamwambia Farao, Jambo hili ni kidole cha Mungu; na moyo wake Farao ukawa mgumu asiwasikilize; vile vile kama BWANA alivyonena.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Wale wachawi wakamwambia Farao, “Hii ni kazi ya mkono wa Mungu.” Lakini moyo wa Farao ukaendelea kuwa mgumu; wala hakuwasikiliza Mose na Aroni. Ikawa kama Mwenyezi-Mungu alivyokuwa amesema.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ndipo, walipomwambia Farao: Hiki ndicho kidole chake Mungu! Lakini moyo wake Farao ukashupaa, asiwasikie, kama Bwana alivyosema.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Ndipo wale waganga wakamwambia Farao, Jambo hili ni chanda cha Mungu; na moyo wake Farao ukawa mgumu asiwasikize; vile vile kama BWANA alivyonena.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Nitakinga watu wangu na mambo yatakayowapata watu wako. Mambo hayo yatafanyika kesho.’ ”