Exodus 8:20 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kisha Mwenyezi-Mungu akamwambia Mose, “Kesho amka asubuhi mapema umwendee Farao wakati anapokwenda mtoni umwambie, ‘Mwenyezi-Mungu asema hivi: Waache watu wangu waondoke ili wanitumikie.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kisha Mwenyezi Mungu akamwambia Musa, “Amka asubuhi na mapema, usimame mbele ya Farao wakati anapoenda mtoni, umwambie, ‘Hili ndilo asemalo Mwenyezi Mungu: Waachie watu wangu waende, ili wapate kuniabudu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Bwana akamwambia Musa, Inuka asubuhi na mapema usimame mbele ya Farao; angalia! Atoka aende majini; kamwambie, Bwana asema, Wape watu wangu ruhusa waende zao, ili wanitumikie mimi.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kisha Mwenyezi-Mungu akamwambia Mose, “Kesho amka asubuhi mapema umwendee Farao wakati anapokwenda mtoni umwambie, ‘Mwenyezi-Mungu asema hivi: waache watu wangu waondoke ili wanitumikie.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kisha BWANA akamwambia Mose, “Amka mapema asubuhi na usimame mbele ya Farao wakati anapokwenda mtoni nawe umwambie, ‘Hili ndilo BWANA asemalo: Waachie watu wangu waende, ili wapate kuniabudu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kisha bwana akamwambia Musa, “Amka mapema asubuhi na usimame mbele ya Farao wakati anapokwenda mtoni nawe umwambie, ‘Hili ndilo bwana asemalo: Waachie watu wangu waende, ili wapate kuniabudu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
BWANA akamwambia Musa, Inuka asubuhi na mapema usimame mbele ya Farao; angalia! Atoka aende majini; kamwambie, BWANA asema, Wape watu wangu ruhusa waende zao, ili wanitumikie mimi.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kisha Mwenyezi-Mungu akamwambia Mose, “Kesho amka asubuhi mapema umwendee Farao wakati anapokwenda mtoni umwambie, ‘Mwenyezi-Mungu asema hivi: Waache watu wangu waondoke ili wanitumikie.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Bwana akamwambia Mose: Kesho asubuhi na mapema ujidamke, upate kumtokea Farao, utakapomwona, akitoka kwenda majini! Ndipo umwambie: Hivi ndivyo, Bwana anavyosema: Watu hawa walio ukoo wangu wape ruhusa kwenda zao, wanitumikie!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
BWANA akamwambia Musa, Inuka asubuhi na mapema usimame mbele ya Farao; angalia! Atoka aende majini; kamwambie, BWANA asema, Wape watu wangu ruhusa waende zao, ili wanitumikie mimi.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Yawe akafanya kama vile alivyosema. Makundi makubwa ya mainzi yakashambulia nyumba ya mufalme wa Misri, nyumba za wakubwa wake na inchi nzima ya Misri. Inchi nzima ya Misri ikaharibiwa na mainzi wale.