Exodus 8:22 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Lakini siku hiyo sehemu ya Gosheni wanakoishi watu wangu nitaikinga: Humo nzi hao hawatakuwamo. Hapo ndipo utakapotambua kwamba mimi Mwenyezi-Mungu natenda mambo nchini mwako.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“ ‘Lakini siku ile nitafanya kitu tofauti katika nchi ya Gosheni, ambapo watu wangu wanaishi, hapatakuwa na makundi ya inzi, ili mpate kujua kwamba Mimi, Mwenyezi Mungu, niko katika nchi hii.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Nami siku hiyo nitatenga nchi ya Gosheni, watu wangu wanayokaa, ili hao mainzi wasiwe huko; ili kwamba upate kujua wewe ya kuwa mimi ndimi Bwana kati ya dunia.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Lakini siku hiyo sehemu ya Gosheni wanakoishi watu wangu nitaikinga: humo nzi hao hawatakuwamo. Hapo ndipo utakapotambua kwamba mimi Mwenyezi-Mungu natenda mambo nchini mwako.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“ ‘Lakini siku ile nitafanya kitu tofauti katika nchi ya Gosheni, ambapo watu wangu wanaishi, hapatakuwepo na makundi ya mainzi, ili mpate kujua kwamba Mimi, BWANA, niko katika nchi hii.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“ ‘Lakini siku ile nitafanya kitu tofauti katika nchi ya Gosheni, ambapo watu wangu wanaishi, hapatakuwepo na makundi ya mainzi, ili mpate kujua kwamba Mimi, bwana, niko katika nchi hii.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Nami siku hiyo nitatenga nchi ya Gosheni, watu wangu wanayokaa, ili hao inzi wasiwe huko; ili kwamba upate kujua wewe ya kuwa mimi ndimi BWANA kati ya dunia.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Lakini siku hiyo sehemu ya Gosheni wanakoishi watu wangu nitaikinga: Humo nzi hao hawatakuwamo. Hapo ndipo utakapotambua kwamba mimi Mwenyezi-Mungu natenda mambo nchini mwako.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Lakini nchi ya Goseni, wao walio ukoo wangu wanayoikaa, nitaitenga siku hiyo, hao mainzi wabaya wasiweko huko, kusudi upate kujua, ya kuwa mimi Bwana niko katikati ya nchi hiyo.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Nami siku hiyo nitatenga nchi ya Gosheni, watu wangu wanayokaa, ili hao mainzi wasiwe huko; ili kwamba upate kujua wewe ya kuwa mimi ndimi BWANA kati ya dunia.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Lakini Musa akamujibu: “Hapana! Haifai kufanya hivyo, maana sadaka tutakazomutolea Yawe, Mungu wetu, zitawachukiza Wamisri. Wamisri wakituona tunatoa sadaka ambazo ni chukizo kwao, si watatupiga mawe?