Exodus 8:25 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Ndipo Farao akawaita Mose na Aroni, akasema, “Mnaweza kwenda kumtambikia Mungu wenu, lakini iwe humuhumu nchini Misri.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Ndipo Farao akamwita Musa na Haruni na kuwaambia, “Nendeni mkamtolee Mungu wenu dhabihu katika nchi hii.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Farao akawaita Musa na Haruni akawaambia, Endeni mkamtolee Mungu wenu dhabihu ndani ya nchi hii.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Ndipo Farao akawaita Mose na Aroni, akasema, “Mnaweza kwenda kumtambikia Mungu wenu, lakini iwe humuhumu nchini Misri.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Ndipo Farao akamwita Mose na Aroni na kuwaambia, “Nendeni mkamtolee Mungu wenu dhabihu katika nchi hii.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Ndipo Farao akamwita Musa na Haruni na kuwaambia, “Nendeni mkamtolee Mungu wenu dhabihu katika nchi hii.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Farao akawaita Musa na Haruni akawaambia, Endeni mkamtolee Mungu wenu dhabihu ndani ya nchi hii.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Ndipo Farao akawaita Mose na Aroni, akasema, “Mnaweza kwenda kumtambikia Mungu wenu, lakini iwe humuhumu nchini Misri.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ndipo, Farao alipomwita Mose na Haroni, akawaambia: Nendeni kumtambikia Mungu wenu katika nchi hii!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Farao akawaita Musa na Haruni akawaambia, Endeni mkamtolee Mungu wenu dhabihu ndani ya nchi hii.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Musa akamujibu: “Mara tu nitakapokuacha, kesho nitamwomba Yawe makundi haya ya mainzi yatoweke kwako wewe mufalme, wakubwa wako na watu wako. Lakini wewe usitudanganye tena kwa kukataa kuwaacha watu kwenda kutoa sadaka kwa Yawe.”