Exodus 8:28 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Basi, Farao akasema, “Nitawaacha mwende zenu kumtambikia Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu, jangwani. Walakini msiende mbali mno. Niombeeni na mimi.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Farao akamwambia, “Nitawaruhusu mwende kumtolea Mwenyezi Mungu, Mungu wenu, dhabihu huko jangwani, lakini hamna ruhusa kwenda mbali sana. Sasa mniombee.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Farao akasema, Mimi nitawapa ruhusa mwende, ili mmchinjie dhabihu Bwana, Mungu wenu, jangwani; lakini hamtakwenda mbali sana; haya niombeeni.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Basi, Farao akasema, “Nitawaacha mwende zenu kumtambikia Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu, jangwani. Walakini msiende mbali mno. Niombeeni na mimi.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Farao akamwambia, “Nitawaruhusu mwende kumtolea BWANA Mungu wenu dhabihu huko jangwani, lakini hamna ruhusa kwenda mbali sana. Sasa mniombee.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Farao akamwambia, “Nitawaruhusu mwende kumtolea bwana Mwenyezi Mungu wenu dhabihu huko jangwani, lakini hamna ruhusa kwenda mbali sana. Sasa mniombee.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Farao akasema, Mimi nitawapa ruhusa mwende, ili mumchinjie dhabihu BWANA, Mungu wenu, jangwani; lakini hamtakwenda mbali sana; haya niombeeni.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Basi, Farao akasema, “Nitawaacha mwende zenu kumtambikia Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu, jangwani. Walakini msiende mbali mno. Niombeeni na mimi.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ndipo, Farao aliposema: Basi, mimi nitawapa ninyi ruhusa kwenda kumtambikia Bwana Mungu wenu nyikani. Ninataka hili tu: msiende mbali zaidi, tena: mniombee.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Farao akasema, Mimi nitawapa ruhusa mwende, ili mmchinjie dhabihu BWANA, Mungu wenu, jangwani; lakini hamtakwenda mbali sana; haya niombeeni.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Lakini hata mara hii mufalme wa Misri akafanya moyo wake kuwa magumu, wala hakuwaruhusu Waisraeli kuondoka.