Exodus 8:29 — Compare Translations
10 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mose akamjibu, “Mara tu nitakapokuacha, nitamwomba Mwenyezi-Mungu makundi haya ya nzi yatoweke kwako wewe Farao, maofisa wako na watu wako, kesho. Lakini wewe usitudanganye tena kwa kukataa kuwaacha watu kwenda kumtambikia Mwenyezi-Mungu.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Musa akajibu, “Mara tu nitakapoondoka, nitamwomba Mwenyezi Mungu na kesho inzi wataondoka kwa Farao, kwa maafisa wake, na kwa watu wake. Ila hakikisha kwamba Farao hatatenda kwa udanganyifu tena kwa kutokuwaachia watu waende kumtolea Mwenyezi Mungu dhabihu.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Musa akasema, Tazama, mimi natoka kwako, nami nitamwomba Bwana ili hao mainzi wamtoke Farao, na watumishi wake, na watu wake kesho; lakini Farao asitende kwa udanganyifu tena, kwa kutowaacha watu waende kumchinjia Bwana dhabihu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mose akamjibu, “Mara tu nitakapokuacha, nitamwomba Mwenyezi-Mungu makundi haya ya nzi yatoweke kwako wewe Farao, maofisa wako na watu wako, kesho. Lakini wewe usitudanganye tena kwa kukataa kuwaacha watu kwenda kumtambikia Mwenyezi-Mungu.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Mose akajibu, “Mara tu nitakapoondoka, nitamwomba BWANA na kesho mainzi yataondoka kwa Farao, kwa maafisa wake na kwa watu wake. Hakikisha tu kwamba Farao hatatenda kwa udanganyifu tena kwa kutokuwaachia watu waende kumtolea BWANA dhabihu.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Musa akajibu, “Mara tu nitakapoondoka, nitamwomba bwana na kesho mainzi yataondoka kwa Farao, kwa maafisa wake na kwa watu wake. Hakikisha tu kwamba Farao hatatenda kwa udanganyifu tena kwa kutokuwaachia watu waende kumtolea bwana dhabihu.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Musa akasema, Tazama, mimi natoka kwako, nami nitamwomba BWANA ili hao inzi wamtoke Farao, na watumishi wake, na watu wake kesho; lakini Farao asitende kwa udanganyifu tena, kwa kutowaacha watu waende kumchinjia BWANA dhabihu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mose akamjibu, “Mara tu nitakapokuacha, nitamwomba Mwenyezi-Mungu makundi haya ya nzi yatoweke kwako wewe Farao, maofisa wako na watu wako, kesho. Lakini wewe usitudanganye tena kwa kukataa kuwaacha watu kwenda kumtambikia Mwenyezi-Mungu.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Naye Mose akasema: Tazama! Nikitoka kwako nitamwomba Bwana, hawa mainzi wabaya waondoke kesho kwake Farao nako kwao watumishi wake na watu wake, lakini Farao asiendelee kutudanganya, akikataa tena kuwapa hawa watu ruhusa kwenda zao, wapate kumtambikia Bwana!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Musa akasema, Tazama, mimi natoka kwako, nami nitamwomba BWANA ili hao mainzi wamtoke Farao, na watumishi wake, na watu wake kesho; lakini Farao asitende kwa udanganyifu tena, kwa kutowaacha watu waende kumchinjia BWANA dhabihu.