Exodus 8:8 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kisha Farao akamwita Mose na Aroni, akamwambia, “Msihi Mwenyezi-Mungu, ili aniondolee mimi na watu wangu vyura hawa, nami nitawaacha Waisraeli waende zao na kumtambikia Mwenyezi-Mungu.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Ndipo Farao akamwita Musa na Haruni na kusema, “Mwombeni Mwenyezi Mungu awaondoe vyura kutoka kwangu na kwa watu wangu, nami nitawaachia watu wenu waende kumtolea Mwenyezi Mungu dhabihu.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Ndipo Farao akawaita Musa na Haruni na kuwaambia, Mwombeni Bwana, ili awaondoe vyura hawa kwangu mimi na kwa watu wangu; nami nitawapa watu ruhusa waende zao, ili wamtolee Bwana dhabihu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kisha Farao akamwita Mose na Aroni, akamwambia, “Msihi Mwenyezi-Mungu, ili aniondolee mimi na watu wangu vyura hawa, nami nitawaacha Waisraeli waende zao na kumtambikia Mwenyezi-Mungu.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Ndipo Farao akamwita Mose na Aroni na kusema, “Mwombeni BWANA awaondoe vyura kutoka kwangu na kwa watu wangu, nami nitawaachia watu wenu waende kumtolea BWANA dhabihu.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Ndipo Farao akamwita Musa na Haruni na kusema, “Mwombeni bwana awaondoe vyura kutoka kwangu na kwa watu wangu, nami nitawaachia watu wenu waende kumtolea bwana dhabihu.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Ndipo Farao akawaita Musa na Haruni na kuwaambia, Mwombeni BWANA, ili awaondoe vyura hawa kwangu mimi na kwa watu wangu; nami nitawapa watu ruhusa waende zao, ili wamtolee BWANA dhabihu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kisha Farao akamwita Mose na Aroni, akamwambia, “Msihi Mwenyezi-Mungu, ili aniondolee mimi na watu wangu vyura hawa, nami nitawaacha Waisraeli waende zao na kumtambikia Mwenyezi-Mungu.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ndipo, Farao alipomwita Mose na Haroni, akawaambia: Niombeeni kwa Bwana, awaondoe hawa vyura kwangu na kwa watu wangu! Ndipo, nitakapowapa ruhusa watu wa ukoo huu kwenda zao, wamtambikie Bwana.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Ndipo Farao akawaita Musa na Haruni na kuwaambia, Mwombeni BWANA, ili awaondoe vyura hawa kwangu mimi na kwa watu wangu; nami nitawapa watu ruhusa waende zao, ili wamtolee BWANA dhabihu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Basi, Musa na Haruni wakaondoka kwa nyumba ya mufalme wa Misri na Musa akamulilia Yawe amwondolee mufalme vyura wale aliomuletea.