Exodus 9:13 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kisha, Mwenyezi-Mungu akamwambia Mose, “Kesho, amka alfajiri na mapema umwendee Farao, umwambie kwamba mimi Mwenyezi-Mungu, Mungu wa Waebrania, nasema hivi, ‘Waache watu wangu waondoke ili wakanitumikie.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kisha Mwenyezi Mungu akamwambia Musa, “Amka asubuhi na mapema, usimame mbele ya Farao, umwambie, ‘Hili ndilo asemalo Mwenyezi Mungu, Mungu wa Waebrania: Waachie watu wangu waende, ili waweze kuniabudu,
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Bwana akamwambia Musa, Ondoka asubuhi na mapema, ukasimame mbele ya Farao, umwambie, Bwana, Mungu wa Waebrania, asema, Wape watu wangu ruhusa waende ili wanitumikie.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kisha, Mwenyezi-Mungu akamwambia Mose, “Kesho, amka alfajiri na mapema umwendee Farao, umwambie kwamba mimi Mwenyezi-Mungu, Mungu wa Waebrania, nasema hivi, ‘Waache watu wangu waondoke ili wakanitumikie.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kisha BWANA akamwambia Mose, “Amka mapema asubuhi, usimame mbele ya Farao, umwambie, ‘Hili ndilo asemalo BWANA, Mungu wa Waebrania: Waachie watu wangu waende, ili kwamba waweze kuniabudu,
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kisha bwana akamwambia Musa, “Amka mapema asubuhi, usimame mbele ya Farao, umwambie, ‘Hili ndilo asemalo bwana, Mungu wa Waebrania: Waachie watu wangu waende, ili kwamba waweze kuniabudu,
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
BWANA akamwambia Musa, Ondoka asubuhi na mapema, ukasimame mbele ya Farao, umwambie, BWANA, Mungu wa Waebrania, asema, Wape watu wangu ruhusa waende ili wanitumikie.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kisha, Mwenyezi-Mungu akamwambia Mose, “Kesho, amka alfajiri na mapema umwendee Farao, umwambie kwamba mimi Mwenyezi-Mungu, Mungu wa Waebrania, nasema hivi, ‘Waache watu wangu waondoke ili wakanitumikie.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Bwana akamwambia Mose: Kesho asubuhi na mapema ujidamke, upate kumtokea Farao na kumwambia: Hivi ndivyo, anavyosema Bwana Mungu wa Waebureo: Watu hawa walio ukoo wangu wape ruhusa kwenda zao!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
BWANA akamwambia Musa, Ondoka asubuhi na mapema, ukasimame mbele ya Farao, umwambie, BWANA, Mungu wa Waebrania, asema, Wape watu wangu ruhusa waende ili wanitumikie.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kisha, Yawe akamwambia Musa: “Kesho, amuka asubui mapema umwendee mufalme wa Misri, umwambie kwamba mimi Yawe, Mungu wa Waebrania, ninasema hivi: ‘Uwaache watu wangu waondoke kusudi wanitumikie.