Exodus 9:20 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Baadhi ya maofisa wa Farao waliyatia maanani maneno hayo ya Mwenyezi-Mungu, wakawapeleka watumwa na wanyama wao nyumbani mahali pa usalama.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Wale maafisa wa Farao ambao waliliogopa neno la Mwenyezi Mungu wakafanya haraka kuwaleta watumwa wao na mifugo yao ndani.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Yeye aliyelicha neno la Bwana miongoni mwa watumishi wa Farao aliwakimbiza watumishi wake na wanyama wake waingie nyumbani;
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Baadhi ya maofisa wa Farao waliyatia maanani maneno hayo ya Mwenyezi-Mungu, wakawapeleka watumwa na wanyama wao nyumbani mahali pa usalama.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Wale maafisa wa Farao ambao waliliogopa neno la BWANA wakafanya haraka kuwaleta watumwa wao na mifugo yao ndani.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Wale maafisa wa Farao ambao waliliogopa neno la bwana wakafanya haraka kuwaleta watumwa wao na mifugo yao ndani.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Yeye aliyelicha neno la BWANA miongoni mwa watumishi wa Farao aliwakimbiza watumishi wake na wanyama wake waingie nyumbani;
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Baadhi ya maofisa wa Farao waliyatia maanani maneno hayo ya Mwenyezi-Mungu, wakawapeleka watumwa na wanyama wao nyumbani mahali pa usalama.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ndipo, wao walioliogopa hilo neno la Bwana miongoni mwa watumishi wa Farao walipowakimbiza watumwa wao na makundi yao na kuwingiza nyumbani.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Yeye aliyelicha neno la BWANA miongoni mwa watumishi wa Farao aliwakimbiza watumishi wake na wanyama wake waingie nyumbani;
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Wakubwa wamoja wa mufalme wa Misri wakaogopa maneno hayo ya Yawe, wakawapeleka watumwa na nyama wao ndani ya nyumba pahali pa usalama.