Exodus 9:22 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kisha, Mwenyezi-Mungu akamwambia Mose, “Nyosha mkono wako juu mbinguni, ili mvua ya mawe inyeshe kila mahali nchini Misri. Imnyeshee mtu, mnyama na kila mmea shambani.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Ndipo Mwenyezi Mungu akamwambia Musa, “Nyoosha mkono wako kuelekea angani ili mvua ya mawe inyeshe Misri yote: juu ya watu, wanyama, na juu ya kila kitu kinachoota katika mashamba ya Misri.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Bwana akamwambia Musa, Nyosha mkono wako kuelekea mbinguni, ili iwe mvua ya mawe katika nchi yote ya Misri, juu ya wanadamu na juu ya wanyama, na juu ya mboga zote za mashamba, katika nchi yote ya Misri.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kisha, Mwenyezi-Mungu akamwambia Mose, “Nyosha mkono wako juu mbinguni, ili mvua ya mawe inyeshe kila mahali nchini Misri. Imnyeshee mtu, mnyama na kila mmea shambani.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Ndipo BWANA akamwambia Mose, “Nyosha mkono wako kuelekea angani ili kwamba mvua ya mawe inyeshe juu ya Misri yote, juu ya watu, wanyama na juu ya kila kitu kiotacho katika mashamba ya Misri.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Ndipo bwana akamwambia Musa, “Nyoosha mkono wako kuelekea angani ili kwamba mvua ya mawe inyeshe juu ya Misri yote, juu ya watu, wanyama na juu ya kila kitu kiotacho katika mashamba ya Misri.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
BWANA akamwambia Musa, Nyosha mkono wako kuelekea mbinguni, ili iwe mvua ya mawe katika nchi yote ya Misri, juu ya wanadamu na juu ya wanyama, na juu ya mboga zote za mashambani, katika nchi yote ya Misri.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kisha, Mwenyezi-Mungu akamwambia Mose, “Nyosha mkono wako juu mbinguni, ili mvua ya mawe inyeshe kila mahali nchini Misri. Imnyeshee mtu, mnyama na kila mmea shambani.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kisha Bwana akamwambia Mose: Unyoshe mkono wako na kuuelekeza mbinguni, mvua ya mawe inyeshe katika nchi yote ya Misri na kuwapiga watu na nyama na majani yote yaliyoko mashambani katika nchi ya Misri!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
BWANA akamwambia Musa, Nyosha mkono wako kuelekea mbinguni, ili iwe mvua ya mawe katika nchi yote ya Misri, juu ya wanadamu na juu ya wanyama, na juu ya mboga zote za mashamba, katika nchi yote ya Misri.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kisha, Yawe akamwambia Musa: “Nyoosha mukono wako juu mbinguni, kusudi mvua ya mawe inyeshe kila pahali katika inchi ya Misri. Imunyeshee mutu, nyama na kila mumea katika shamba.”