Exodus 9:28 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mwombeni Mwenyezi-Mungu kwani ngurumo hii na mvua ya mawe vimezidi. Mimi nitawaacheni mwondoke na wala hamtakaa tena zaidi.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Mwombeni Mwenyezi Mungu, kwa kuwa tumepata ngurumo na mvua za mawe za kutosha. Nitawaachia mwondoke; hamtahitaji kungoja zaidi.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Mwombeni Bwana; kwa kuwa zimekuwa za kutosha ngurumo hizo kuu na hii mvua ya mawe; nami nitawapa ninyi ruhusa mwende zenu, msikae zaidi.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mwombeni Mwenyezi-Mungu kwani ngurumo hii na mvua ya mawe vimezidi. Mimi nitawaacheni mwondoke na wala hamtakaa tena zaidi.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Mwombeni BWANA, kwa kuwa tumepata ngurumo na mvua za mawe za kututosha. Nitawaachia mwondoke; hamtahitaji kungoja zaidi.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Mwombeni bwana, kwa kuwa tumepata ngurumo na mvua za mawe za kututosha. Nitawaachia mwondoke; hamtahitaji kungoja zaidi.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Mwombeni BWANA; kwa kuwa zimekuwa za kutosha ngurumo hizo kuu na hii mvua ya mawe; nami nitawapa ninyi ruhusa mwende zenu, msikae zaidi.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mwombeni Mwenyezi-Mungu kwani ngurumo hii na mvua ya mawe vimezidi. Mimi nitawaacheni mwondoke na wala hamtakaa tena zaidi.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Niombeeni kwa Bwana, hizi ngurumo za Mungu zikome pamoja na mvua ya mawe kwa kuwa nyingi mno! Kisha nitawapa ninyi ruhusa kwenda zenu, msikae huku tena siku nyingi.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Mwombeni BWANA; kwa kuwa zimekuwa za kutosha ngurumo hizo kuu na hii mvua ya mawe; nami nitawapa ninyi ruhusa mwende zenu, msikae zaidi.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Mumwombe Yawe maana ngurumo hii na mvua ya mawe vimezidi. Mimi nitawaacha muondoke na wala hamutabakia tena.”