Exodus 9:3 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
nitaunyosha mkono wangu na kuleta maradhi mabaya sana juu ya mifugo yenu yote: Ng'ombe, farasi, punda, ngamia, mbuzi na kondoo.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
mkono wa Mwenyezi Mungu utaleta pigo baya kwa mifugo yako, juu ya farasi wako, punda, ngamia, ng’ombe wako, kondoo na mbuzi.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
tazama, mkono wa Bwana u juu ya wanyama wako wa mifugo walioko kondeni, juu ya farasi, na juu ya punda, na juu ya ngamia, na juu ya ng'ombe, na juu ya kondoo; kutakuwa na tauni nzito sana.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
nitaunyosha mkono wangu na kuleta maradhi mabaya sana juu ya mifugo yenu yote: ng'ombe, farasi, punda, ngamia, mbuzi na kondoo.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
mkono wa BWANA utaleta pigo baya kwa mifugo yako, juu ya farasi wako, punda, ngamia, ng'ombe wako, kondoo na mbuzi.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
mkono wa bwana utaleta pigo baya kwa mifugo yako, juu ya farasi wako, punda, ngamia, ng’ombe wako, kondoo na mbuzi.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
tazama, mkono wa BWANA uko juu ya wanyama wako wa mifugo walioko kondeni, juu ya farasi, na juu ya punda, na juu ya ngamia, na juu ya ng'ombe, na juu ya kondoo; kutakuwa na tauni nzito sana.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
nitaunyosha mkono wangu na kuleta maradhi mabaya sana juu ya mifugo yenu yote: Ng'ombe, farasi, punda, ngamia, mbuzi na kondoo.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
ndipo, utakapouona mkono wa Bwana, ukiyajia makundi ya mashambani, farasi na punda na ngamia na ng'ombe na mbuzi na kondoo, wapatwe na kidei kikali sana.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
tazama, mkono wa BWANA u juu ya wanyama wako wa mifugo walioko kondeni, juu ya farasi, na juu ya punda, na juu ya ngamia, na juu ya ng’ombe, na juu ya kondoo; kutakuwa na tauni nzito sana.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
nitanyoosha mukono wangu na kuleta ugonjwa mukali sana juu ya nyama wenu wote: ngombe, farasi, punda, ngamia, mbuzi na kondoo.