Ezekiel 1:10 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kuhusu nyuso zao nne kila mmoja wao alikuwa na uso wa binadamu upande wa mbele, uso wa simba upande wa kulia, uso wa ng'ombe upande wa kushoto, na uso wa tai upande wa nyuma.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kuonekana kwa nyuso zao kulikuwa hivi: Kila mmoja wa hao wanne alikuwa na uso wa mwanadamu, na kwa upande wa kulia kila mmoja alikuwa na uso wa simba, na kwa upande wa kushoto alikuwa na uso wa ng’ombe; pia kila mmoja alikuwa na uso wa tai.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kwa habari za mfano wa nyuso zao; walikuwa na uso wa mwanadamu; na hao wanne walikuwa na uso wa simba upande wa kuume; na hao wanne walikuwa na uso wa ng'ombe upande wa kushoto; na hao wanne walikuwa na uso wa tai pia.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kuhusu nyuso zao nne kila mmoja wao alikuwa na uso wa binadamu upande wa mbele, uso wa simba upande wa kulia, uso wa ng'ombe upande wa kushoto, na uso wa tai upande wa nyuma.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kuonekana kwa nyuso zao kulikuwa hivi: Kila mmoja wa wale wanne alikuwa na uso wa mwanadamu na kwa upande wa kulia kila mmoja alikuwa na uso wa simba, upande wa kushoto alikuwa na uso wa ng'ombe pia kila mmoja alikuwa na uso wa tai.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kuonekana kwa nyuso zao kulikuwa hivi: Kila mmoja wa wale wanne alikuwa na uso wa mwanadamu na kwa upande wa kulia kila mmoja alikuwa na uso wa simba, upande wa kushoto alikuwa na uso wa ng’ombe pia kila mmoja alikuwa na uso wa tai.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kwa habari za mfano wa nyuso zao; walikuwa na uso wa mwanadamu; na hao wanne walikuwa na uso wa simba upande wa kulia; na hao wanne walikuwa na uso wa ng'ombe upande wa kushoto; na hao wanne walikuwa na uso wa tai pia.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kuhusu nyuso zao nne kila mmoja wao alikuwa na uso wa binadamu upande wa mbele, uso wa simba upande wa kulia, uso wa ng'ombe upande wa kushoto, na uso wa tai upande wa nyuma.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Nyuso zao mifano yao ilikuwa hivyo: mbele ni uso wa mtu, kuumeni kwao hao wanne ni uso wa simba, kushotoni kwao hao wanne ni uso wa ng'ombe, tena kwao hao wanne nyuma yao ni uso wa tai.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kwa habari za mfano wa nyuso zao; walikuwa na uso wa mwanadamu; na hao wanne walikuwa na uso wa simba upande wa kuume; na hao wanne walikuwa na uso wa ng’ombe upande wa kushoto; na hao wanne walikuwa na uso wa tai pia.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Juu ya nyuso zao: kila kimoja kilikuwa na uso wa mutu upande wa mbele, uso wa simba upande wa kuume, uso wa ngombe upande wa kushoto, na uso wa tai upande wa nyuma.