Ezekiel 1:11 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mabawa mawili ya kila mmoja yalikuwa yamekunjuliwa juu na kugusana na kwa mabawa yale mengine mawili walifunika miili yao.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Hivyo ndivyo zilivyokuwa nyuso zao. Kila mmoja wao alikuwa na mabawa mawili yaliokunjuliwa kuelekea juu; kila bawa liligusa bawa la mwenzake kila upande; kila mmoja wao alikuwa na mabawa mawili yaliyofunika mwili wake.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na nyuso zao na mabawa yao yalikuwa yametengana kwa juu; mabawa mawili ya kila mmoja yaliungana, hili na hili, na mawili yalifunika miili yao.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mabawa mawili ya kila mmoja yalikuwa yamekunjuliwa juu na kugusana na kwa mabawa yale mengine mawili walifunika miili yao.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Hivyo ndivyo zilivyokuwa nyuso zao. Mabawa yao yalikunjuliwa kuelekea juu, kila mmoja alikuwa na mabawa mawili ambayo kila moja liligusa bawa la mwenzake kila upande na mabawa mengine mawili yakifunika mwili wake.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Hivyo ndivyo zilivyokuwa nyuso zao. Mabawa yao yalikunjuliwa kuelekea juu, kila mmoja alikuwa na mabawa mawili ambayo kila moja liligusa bawa la mwenzake kila upande na mabawa mengine mawili yakifunika mwili wake.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na nyuso zao na mabawa yao yalikuwa yametengana kwa juu; mabawa mawili ya kila mmoja yaliungana, hili na hili, na mawili yalifunika miili yao.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mabawa mawili ya kila mmoja yalikuwa yamekunjuliwa juu na kugusana na kwa mabawa yale mengine mawili walifunika miili yao.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Nayo mabawa yao yalikuwa yamejitanda juu, kwake kila mmoja mawili yalishikana, mawili yaliifunika miili yao.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na nyuso zao na mabawa yao yalikuwa yametengana kwa juu; mabawa mawili ya kila mmoja yaliungana, hili na hili, na mawili yalifunika miili yao.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Mabawa mawili ya kila kimoja yalikuwa yamekunjuliwa juu na kugusana; na kwa mabawa yale mengine mawili, vilifunika miili yao.