Ezekiel 1:16 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Magurudumu hayo yalionekana kuwa ya namna moja, yanametameta kama jiwe la zabarajadi na muundo wao ulikuwa kama gurudumu ndani ya gurudumu lingine.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Hivi ndivyo ilivyokuwa kuonekana kwa hayo magurudumu na muundo wake: yalimetameta kama zabarajadi, nayo yote manne yalifanana. Kila gurudumu lilionekana kuwa na gurudumu lingine ndani yake.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kuonekana kwake magurudumu hayo na kazi yake kulikuwa kama rangi ya zabarajadi; nayo yote manne yalikuwa na mfano mmoja; na kuonekana kwake na kazi yake kulikuwa kana kwamba ni gurudumu ndani ya gurudumu lingine.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Magurudumu hayo yalionekana kuwa ya namna moja, yanametameta kama jiwe la zabarajadi na muundo wao ulikuwa kama gurudumu ndani ya gurudumu lingine.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Hivi ndivyo ilivyokuwa kuonekana kwa hayo magurudumu na muundo wake: yaling'aa kama zabarajadi, nayo yote manne yalifanana. Kila gurudumu lilikuwa na gurudumu jingine ndani yake.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Hivi ndivyo ilivyokuwa kuonekana kwa hayo magurudumu na muundo wake: yaling’aa kama zabarajadi, nayo yote manne yalifanana. Kila gurudumu lilikuwa na gurudumu jingine ndani yake.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kuonekana kwake magurudumu hayo na kazi yake kulikuwa kama rangi ya zabarajadi; nayo yote manne yalikuwa na mfano mmoja; na kuonekana kwake na kazi yake kulikuwa kana kwamba ni gurudumu ndani ya gurudumu lingine.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Magurudumu hayo yalionekana kuwa ya namna moja, yanametameta kama jiwe la zabarajadi na muundo wao ulikuwa kama gurudumu ndani ya gurudumu lingine.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Nilipoyatazama hayo magurudumu, jinsi yalivyotengenezwa, jinsi yalivyokuwa, yalikuwa kama kito cha Tarsisi, yote manne mfano wao ulikuwa huo mmoja; nilipoyatazama tena, jinsi yalivyotengenezwa, yalionekana kuwa kama gurudumu moja lililomo ndani ya gurudumu lenziwe.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kuonekana kwake magurudumu hayo na kazi yake kulikuwa kama rangi ya zabarajadi; nayo yote manne yalikuwa na mfano mmoja; na kuonekana kwake na kazi yake kulikuwa kana kwamba ni gurudumu ndani ya gurudumu lingine.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Magurudumu hayo yalionekana kuwa ya namna moja, yanametameta kama jiwe la zabarajadi na umbo lao lilikuwa kama gurudumu ndani ya gurudumu lingine.