Ezekiel 1:26 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Juu ya kitu hicho niliona kitu kama kiti cha enzi cha johari ya rangi ya samawati. Juu yake aliketi mmoja anayefanana na binadamu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Juu ya ile nafasi ya wazi iliyokuwa juu ya vichwa vyao, kulikuwa na kitu mfano wa kiti cha utawala cha yakuti samawi. Na juu ya kile kiti cha utawala kulikuwa na umbo, mfano wa mwanadamu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na juu ya anga, lililokuwa juu ya vichwa vyao, palikuwa na mfano wa kiti cha enzi, kuonekana kwake kama yakuti samawi; na juu ya mfano huo wa kiti cha enzi, ulikuwako mfano kama kuonekana kwa mfano wa mwanadamu juu yake.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Juu ya kitu hicho niliona kitu kama kiti cha enzi cha johari ya rangi ya samawati. Juu yake aliketi mmoja anayefanana na binadamu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Juu ya ile nafasi ya wazi iliyokuwa juu ya vichwa vyao kulikuwa na kitu mfano wa kiti cha enzi kuonekana kwake chenye rangi ya yakuti samawi, na juu ya kile kiti cha enzi kulikuwa na umbo mfano wa mwanadamu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Juu ya ile nafasi ya wazi iliyokuwa juu ya vichwa vyao kulikuwa na kitu mfano wa kiti cha enzi cha yakuti samawi. Na juu ya kile kiti cha enzi kulikuwa na umbo mfano wa mwanadamu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na juu ya anga, lililokuwa juu ya vichwa vyao, palikuwa na mfano wa kiti cha enzi, kuonekana kwake kama yakuti samawi; na juu ya mfano huo wa kiti cha enzi, ulikuwako mfano kama kuonekana kwa mfano wa mwanadamu juu yake.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Juu ya kitu hicho niliona kitu kama kiti cha enzi cha johari ya rangi ya samawati. Juu yake aliketi mmoja anayefanana na binadamu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Tena juu ya ukingo uliokuwa juu ya vichwa vyao kulionekana kilichokuwa kama kito cha Safiro, nacho kilifanana na kiti cha kifalme; tena katika hicho kilichofanana na kiti cha kifalme kulionekana aliyefanana na mtu, anakikalia.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na juu ya anga, lililokuwa juu ya vichwa vyao, palikuwa na mfano wa kiti cha enzi, kuonekana kwake kama yakuti samawi; na juu ya mfano huo wa kiti cha enzi, ulikuwako mfano kama kuonekana kwa mfano wa mwanadamu juu yake.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Juu ya kitu hicho niliona kitu kimoja kinachofanana na kiti cha kifalme chenye rangi la jiwe la yakuti. Juu yake kulikuwa kunaikaa kitu kinachofanana na mutu.