Ezekiel 1:27 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Sehemu ya juu ya mwili wake ilingaa kama shaba, kama moto uliozunguka pande zote; sehemu ya chini ya mwili wake ilikuwa kama moto nayo ilizungukwa na mngao
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Nikaona kwamba kutokana na kile kilichoonekana kuwa kiuno chake kuelekea juu, alionekana kama chuma inavyong’aa ikiwa ndani ya moto, na kuanzia kiuno kwenda chini alionekana kama moto; mwanga wenye kung’aa sana ulimzunguka.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Nikaona kana kwamba ni rangi ya kaharabu, kama kuonekana kwa moto ndani yake pande zote, tangu kuonekana kwa viuno vyake na juu; na tangu kuonekana kwa viuno vyake na chini, naliona kana kwamba ni kuonekana kwa moto; tena palikuwa na mwangaza pande zake zote.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Sehemu ya juu ya mwili wake iling'aa kama shaba, kama moto uliozunguka pande zote; sehemu ya chini ya mwili wake ilikuwa kama moto nayo ilizungukwa na mng'ao
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Nikaona kwamba kutokana na kile nilichoona kama kiuno chake kuelekea juu alionekana kama chuma inayowaka kana kwamba imejaa moto na kuanzia kiuno kwenda chini alionekana kama moto na mwanga mkali ulimzunguka.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Nikaona kwamba kutokana na kile nilichoona kama kiuno chake kuelekea juu alionekana kama chuma inayowaka kana kwamba imejaa moto na kuanzia kiuno kwenda chini alionekana kama moto na mwanga mkali ulimzunguka.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Nikaona kana kwamba ni rangi ya kaharabu, kama kuonekana kwa moto ndani yake pande zote, tangu kuonekana kwa viuno vyake na juu; na tangu kuonekana kwa viuno vyake na chini, niliona kana kwamba ni kuonekana kwa moto; tena palikuwa na mwangaza pande zake zote.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Sehemu ya juu ya mwili wake ilingaa kama shaba, kama moto uliozunguka pande zote; sehemu ya chini ya mwili wake ilikuwa kama moto nayo ilizungukwa na mngao
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Nilipotazama tena nikaona ndani yake kilichofanana na shaba iliyong'aa sana, kilionekana kuwa kama moto uliofungiwa nyumbani po pote. Tena hapo palipokuwa kama kiuno chake mpaka juu, tena toka hapo palipofanana kuwa kama kiuno chake mpaka chini nilipopatazama nikaona kuwa kama moto uung'aao kabisa po pote.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Nikaona kana kwamba ni rangi ya kaharabu, kama kuonekana kwa moto ndani yake pande zote, tangu kuonekana kwa viuno vyake na juu; na tangu kuonekana kwa viuno vyake na chini, naliona kana kwamba ni kuonekana kwa moto; tena palikuwa na mwangaza pande zake zote.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Sehemu ya juu ya mwili wake ilingaa kama shaba, nao ulikuwa sawa unazungukwa na moto pande zote. Tokea sehemu ya chini ya mwili wake, niliona kitu kama moto. Mwangaza ulimuzunguka.