Ezekiel 1:28 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
ulioonekana kama upinde wakati wa mvua. Ndivyo ulivyoonekana mfano wa utukufu wa Mwenyezi-Mungu. Nilipouona, nilianguka kifudifudi, nikasikia sauti ya mtu anaongea.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kama vile kuonekana kwa upinde wa mvua mawinguni siku ya mvua, ndivyo ulivyokuwa ule mng’ao uliomzunguka. Hivi ndivyo mfano wa utukufu wa Mwenyezi Mungu ulionekana. Nilipouona, nikaanguka kifudifudi, nikasikia sauti ya mtu anaongea.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kama kuonekana kwa upinde wa mvua, ulio katika mawingu siku ya mvua, ndivyo kulivyokuwa kuonekana kwa mwangaza ule pande zote. Ndivyo kulivyokuwa kuonekana kwake mfano huo wa utukufu wa Bwana. Nami nilipoona nalianguka kifudifudi, nikasikia sauti ya mmoja anenaye.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
ulioonekana kama upinde wakati wa mvua. Ndivyo ulivyoonekana mfano wa utukufu wa Mwenyezi-Mungu. Nilipouona, nilianguka kifudifudi, nikasikia sauti ya mtu anaongea.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kama vile kuonekana kwa upinde wa mvua mawinguni siku ya mvua, ndivyo ulivyokuwa ule mng'ao uliomzunguka. Hivi ndivyo ilivyokuwa kuonekana kwa utukufu wa BWANA. Nilipouona, nikaanguka kifudifudi, nikasikia sauti ya mtu anaongea.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kama vile kuonekana kwa upinde wa mvua mawinguni siku ya mvua, ndivyo ulivyokuwa ule mng’ao uliomzunguka. Hivi ndivyo ilivyokuwa kuonekana kwa utukufu wa bwana. Nilipouona, nikaanguka kifudifudi, nikasikia sauti ya mtu anaongea.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kama kuonekana kwa upinde wa mvua, ulio katika mawingu siku ya mvua, ndivyo kulivyokuwa kuonekana kwa mwangaza ule pande zote. Ndivyo kulivyokuwa kuonekana kwake mfano huo wa utukufu wa BWANA. Nami nilipoona nilianguka kifudifudi, nikasikia sauti ya mmoja anenaye.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
ulioonekana kama upinde wakati wa mvua. Ndivyo ulivyoonekana mfano wa utukufu wa Mwenyezi-Mungu. Nilipouona, nilianguka kifudifudi, nikasikia sauti ya mtu anaongea.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ulionekana kuwa kama upindi ulioko mawinguni siku ya mvua, ndivyo, kuangazika kwake kulivyokuwa po pote; huu ndio mfano wa utukufu wake Bwana. Nilipouona, nikaanguka kifudifudi, nikasikia sauti ya mwenye kusema.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kama kuonekana kwa upinde wa mvua, ulio katika mawingu siku ya mvua, ndivyo kulivyokuwa kuonekana kwa mwangaza ule pande zote. Ndivyo kulivyokuwa kuonekana kwake mfano huo wa utukufu wa BWANA. Nami nilipoona nalianguka kifudifudi, nikasikia sauti ya mmoja anenaye.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Ulionekana kama upindi wa mvua wakati wa mvua. Ulionekana kufanana na utukufu wa Yawe. Nilipouona, nilianguka uso mpaka chini, nikasikia sauti ya mutu mwenye kusema.