Ezekiel 1:4 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Nilipotazama niliona upepo wa dhoruba unavuma kutoka kaskazini: Kulikuwa na wingu kubwa lililozungukwa na mngao, na moto ulichomoza humo mfululizo na katikati ya huo moto kulikuwa na kitu kinametameta kama shaba.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Nilitazama, nikaona dhoruba kubwa ikitoka kaskazini: wingu kubwa sana likiwa na miali ya radi, likizungukwa na mwanga mkali. Katikati ya huo moto kulikuwa kama chuma inavyong’aa ndani ya moto.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Nikaona, na tazama, upepo wa dhoruba ulitoka upande wa kaskazini, wingu kubwa sana, pamoja na moto, ukifanya duara ya nuru, na mwangaza pande zote, na katikati yake kitu kama rangi ya kaharabu, katikati ya moto huo.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Nilipotazama niliona upepo wa dhoruba unavuma kutoka kaskazini: kulikuwa na wingu kubwa lililozungukwa na mng'ao, na moto ulichomoza humo mfululizo na katikati ya huo moto kulikuwa na kitu kinametameta kama shaba.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Nilitazama, nikaona dhoruba kubwa ikitoka kaskazini, wingu kubwa sana pamoja likiwa na umeme wa radi likiwa limezungukwa na mwanga mkali. Katikati ya huo moto kulikuwa kama rangi ya manjano ya chuma kinapokuwa ndani ya moto.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Nilitazama, nikaona dhoruba kubwa ikitoka kaskazini, wingu kubwa sana likiwa na umeme wa radi likiwa limezungukwa na mwanga mkali. Katikati ya huo moto kulikuwa kama rangi ya manjano ya chuma kinapokuwa ndani ya moto.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Nikaona, na tazama, upepo wa dhoruba ulitoka upande wa kaskazini, wingu kubwa sana, pamoja na moto, ukifanya duara ya nuru, na mwangaza pande zote, na katikati yake kitu kama rangi ya kaharabu, katikati ya moto huo.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Nilipotazama niliona upepo wa dhoruba unavuma kutoka kaskazini: Kulikuwa na wingu kubwa lililozungukwa na mngao, na moto ulichomoza humo mfululizo na katikati ya huo moto kulikuwa na kitu kinametameta kama shaba.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Nilipotazama nikaona upepo wenye nguvu uliotoka kaskazini na wingu kubwa lililowaka mioto iliyokamatana na kumetameta po pote, namo ndani yake mlikuwamo kilichofanana na shaba iliyong'aa sana mle motoni katikati.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Nikaona, na tazama, upepo wa dhoruba ulitoka upande wa kaskazini, wingu kubwa sana, pamoja na moto, ukifanya duara ya nuru, na mwangaza pande zote, na katikati yake kitu kama rangi ya kaharabu, katikati ya moto huo.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Nilipoangalia niliona upepo wa zoruba unavuma kutokea upande wa kaskazini: kulikuwa wingu kubwa lililozungukwa na mwangaza, na moto ulitokea humo mufululizo na katikati ya huo moto kulikuwa kitu kinachometameta kama shaba.