Ezekiel 10:1 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kisha nikaona kwamba katika lile anga juu ya vichwa vya viumbe wenye mabawa kulikuwa na kitu kinachofanana na johari ya rangi ya samawati, umbo lake kama kiti cha enzi.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Nikatazama, nikaona juu ya ile nafasi iliyokuwa juu ya vichwa vya wale makerubi kulikuwa na kitu mfano wa kiti cha utawala cha yakuti samawi.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Ndipo nikaangalia, na tazama, katika anga lililokuwa juu ya vichwa vya makerubi, kulionekana juu yao kana kwamba ni yakuti samawi, kuonekana kama mfano wa kiti cha enzi.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kisha nikaona kwamba katika lile anga juu ya vichwa vya viumbe wenye mabawa kulikuwa na kitu kinachofanana na johari ya rangi ya samawati, umbo lake kama kiti cha enzi.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Nikatazama, nikaona juu ya ile nafasi iliyokuwa juu ya vichwa vya wale makerubi kulikuwa na kitu kilichofanana na kiti cha enzi cha yakuti samawati.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Nikatazama, nikaona juu ya ile nafasi iliyokuwa juu ya vichwa vya wale makerubi kulikuwa na kitu mfano wa kiti cha enzi cha yakuti samawi.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Ndipo nikaangalia, na tazama, katika anga lililokuwa juu ya vichwa vya makerubi, kulionekana juu yao kana kwamba ni yakuti samawi, kuonekana kama mfano wa kiti cha enzi.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kisha nikaona kwamba katika lile anga juu ya vichwa vya viumbe wenye mabawa kulikuwa na kitu kinachofanana na johari ya rangi ya samawati, umbo lake kama kiti cha enzi.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Nilipotazama penye ukingo uliokuwa juu ya vichwa vyao Makerubi nikaona kilichokuwa kama kito cha Safiro, kikafanana sura yake kuwa kama kiti cha kifalme, kikaonekana kuwa juu yao.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Ndipo nikaangalia, na tazama, katika anga lililokuwa juu ya vichwa vya makerubi, kulionekana juu yao kana kwamba ni yakuti samawi, kuonekana kama mfano wa kiti cha enzi.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kisha nikaona kwamba katika lile anga juu ya vichwa vya makerubi kulikuwa kitu kinachofanana na jiwe la rangi ya samawi, umbo lake kama kiti cha kifalme.