Ezekiel 10:17 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Waliposimama, magurudumu nayo yalisimama; hao walipopaa juu, magurudumu nayo yalipaa pamoja nao. Roho ya hao viumbe ilikuwa pia katika magurudumu hayo.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Makerubi waliposimama, nayo pia yalitulia; nao makerubi walipoinuka juu, magurudumu nayo yaliinuka juu pamoja nao, kwa sababu roho ya wale viumbe hai ilikuwa ndani ya magurudumu hayo.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Waliposimama hao, hayo nayo yalisimama; na walipopaa juu hao, hayo nayo yalipaa juu pamoja nao; maana roho ya huyo kiumbe hai ilikuwa ndani yao.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Waliposimama, magurudumu nayo yalisimama; hao walipopaa juu, magurudumu nayo yalipaa pamoja nao. Roho ya hao viumbe ilikuwa pia katika magurudumu hayo.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Makerubi yaliposimama kimya, nayo pia yalitulia kimya, nao makerubi yalipoinuka juu, magurudumu nayo yaliinuka juu pamoja nao, kwa sababu roho ya vile viumbe hai ilikuwa ndani yake.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Makerubi yaliposimama kimya, nayo pia yalitulia kimya, nao makerubi yalipoinuka juu, magurudumu nayo yaliinuka juu pamoja nao, kwa sababu roho ya vile viumbe hai ilikuwa ndani yake.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Waliposimama hao, hayo nayo yalisimama; na walipopaa juu hao, hayo nayo yalipaa juu pamoja nao; maana roho ya huyo kiumbe hai ilikuwa ndani yao.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Waliposimama, magurudumu nayo yalisimama; hao walipopaa juu, magurudumu nayo yalipaa pamoja nao. Roho ya hao viumbe ilikuwa pia katika magurudumu hayo.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Waliposimama, nayo yakasimama; walipoinuka kwenda juu, nayo yakajiinua kwenda juu pamoja nao, kwani roho ya huyo nyama ilikuwa namo katika hayo magurudumu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Waliposimama hao, hayo nayo yalisimama; na walipopaa juu hao, hayo nayo yalipaa juu pamoja nao; maana roho ya huyo kiumbe hai ilikuwa ndani yao.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Waliposimama, magurudumu nayo yalisimama; hao walipopanda juu, magurudumu nayo yalipanda pamoja nao. Maana roho wa hao viumbe ilikuwa katika magurudumu hayo.