Ezekiel 10:19 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Viumbe wakakunjua mabawa yao, wakapaa juu, mimi nikiwa nawaona na yale magurudumu yalikuwa kando yao. Wakasimama mbele ya lango la mashariki la nyumba ya Mwenyezi-Mungu, na utukufu wa Mungu wa Israeli ulikuwa juu yao.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Nilipokuwa nikitazama, makerubi wakatanda mabawa yao na kuinuka kutoka ardhini, nao walipokuwa wakienda, yale magurudumu yakaenda pamoja nao. Wakasimama kwenye ingilio la lango la mashariki la nyumba ya Mwenyezi Mungu; nao utukufu wa Mungu wa Israeli ukawa juu yao.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Nao makerubi wakainua mabawa yao, wakapaa juu kutoka katika dunia machoni pangu, hapo walipotoka nje, nayo magurudumu yakawa kando yao; wakasimama mahali pa kuingilia pa mlango wa upande wa mashariki wa nyumba ya Bwana; na utukufu wa Mungu wa Israeli ulikuwa juu yao.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Viumbe wakakunjua mabawa yao, wakapaa juu, mimi nikiwa nawaona na yale magurudumu yalikuwa kando yao. Wakasimama mbele ya lango la mashariki la nyumba ya Mwenyezi-Mungu, na utukufu wa Mungu wa Israeli ulikuwa juu yao.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Nilipokuwa nikitazama, makerubi yakatanda mabawa yao na kuinuka kutoka ardhini, nao walipokuwa wakienda yale magurudumu yakaenda pamoja nao. Wakasimama kwenye ingilio la lango la mashariki la nyumba ya BWANA, nao utukufu wa Mungu wa Israeli ukawa juu yao.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Nilipokuwa nikitazama, makerubi yakatanda mabawa yao na kuinuka kutoka ardhini, nao walipokuwa wakienda, yale magurudumu yakaenda pamoja nao. Wakasimama kwenye ingilio la lango la mashariki la nyumba ya bwana, nao utukufu wa Mungu wa Israeli ukawa juu yao.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Nao makerubi wakainua mabawa yao, wakapaa juu kutoka katika dunia machoni pangu, hapo walipotoka nje, nayo magurudumu yakawa kando yao; wakasimama mahali pa kuingilia pa mlango wa upande wa mashariki wa nyumba ya BWANA; na utukufu wa Mungu wa Israeli ulikuwa juu yao.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Viumbe wakakunjua mabawa yao, wakapaa juu, mimi nikiwa nawaona na yale magurudumu yalikuwa kando yao. Wakasimama mbele ya lango la mashariki la nyumba ya Mwenyezi-Mungu, na utukufu wa Mungu wa Israeli ulikuwa juu yao.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Makerubi wakayakunjua mabawa yao, wakaondoka katika nchi kwenda juu machoni pangu; ndivyo, walivyotoka hapo, hayo magurudumu hayo yakawa kandokando yao; wakasimama tena kwenye lango la Nyumba ya Bwana lielekealo maawioni kwa jua, nao utukufu wa Mungu wa Isiraeli ulikuwa juu yao.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Nao makerubi wakainua mabawa yao, wakapaa juu kutoka katika dunia machoni pangu, hapo walipotoka nje, nayo magurudumu yakawa kando yao; wakasimama mahali pa kuingilia pa mlango wa upande wa mashariki wa nyumba ya BWANA; na utukufu wa Mungu wa Israeli ulikuwa juu yao.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Makerubi wakakunjua mabawa yao, wakapanda juu, mimi nikiwa ninawaona na yale magurudumu yalikuwa pembeni yao. Wakasimama mbele ya mulango wa upande wa mashariki wa nyumba ya Yawe, na utukufu wa Mungu wa Israeli ulikuwa juu yao.