Ezekiel 10:4 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Utukufu wa Mwenyezi-Mungu ukapaa juu kutoka kwa wale viumbe wenye mabawa ukaenda kwenye kizingiti cha nyumba hiyo, na lile wingu likaijaza nyumba, na ua ukajaa mngao wa utukufu wa Mwenyezi-Mungu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kisha utukufu wa Mwenyezi Mungu ukainuka kutoka juu ya wale makerubi, ukaenda kwenye kizingiti cha Hekalu. Wingu likajaza Hekalu, nao ukumbi ukajawa na mng’ao wa utukufu wa Mwenyezi Mungu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Utukufu wa Bwana ukapaa kutoka kwa kerubi yule, ukasimama juu ya kizingiti cha nyumba; nayo nyumba ikajazwa na lile wingu, na ua ulikuwa umejaa mwangaza wa utukufu wa Bwana.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Utukufu wa Mwenyezi-Mungu ukapaa juu kutoka kwa wale viumbe wenye mabawa ukaenda kwenye kizingiti cha nyumba hiyo, na lile wingu likaijaza nyumba, na ua ukajaa mng'ao wa utukufu wa Mwenyezi-Mungu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kisha utukufu wa BWANA ukainuka kutoka juu ya wale makerubi ukaenda kwenye kizingiti cha Hekalu. Wingu likajaza Hekalu, nao ukumbi ukajawa na mng'ao wa utukufu wa BWANA.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kisha utukufu wa bwana ukainuka kutoka juu ya wale makerubi ukaenda kwenye kizingiti cha Hekalu. Wingu likajaza Hekalu, nao ukumbi ukajawa na mng’ao wa utukufu wa bwana.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Utukufu wa BWANA ukapaa kutoka kwa kerubi yule, ukasimama juu ya kizingiti cha nyumba; nayo nyumba ikajazwa na lile wingu, na ua ulikuwa umejaa mwangaza wa utukufu wa BWANA.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Utukufu wa Mwenyezi-Mungu ukapaa juu kutoka kwa wale viumbe wenye mabawa ukaenda kwenye kizingiti cha nyumba hiyo, na lile wingu likaijaza nyumba, na ua ukajaa mngao wa utukufu wa Mwenyezi-Mungu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Utukufu wa Bwana ukaondoka kwa Makerubi kwenda penye kizingiti cha kuiingilia hiyo Nyumba, hiyo Nyumba ikajazwa na lile wingu, ua nao ukajaa ung'avu wa utukufu wa Bwana.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Utukufu wa BWANA ukapaa kutoka kwa kerubi yule, ukasimama juu ya kizingiti cha nyumba; nayo nyumba ikajazwa na lile wingu, na ua ulikuwa umejaa mwangaza wa utukufu wa BWANA.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Utukufu wa Yawe ukapanda juu tokea wale makerubi ukaenda kwenye kizingiti cha nyumba hiyo, na lile wingu likaijaza nyumba, na kiwanja kilijaa mwangaza wa utukufu wa Yawe.