Ezekiel 10:7 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kiumbe mmoja akanyosha mkono wake kuchukua moto uliokuwa katikati ya viumbe wenye mabawa, akatwaa sehemu yake na kuutia mikononi mwa yule mtu aliyevaa mavazi ya kitani; naye alipoupokea, akaenda zake.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Ndipo mmoja wa wale makerubi akanyoosha mkono wake kwenye moto uliokuwa katikati yao, akauchukua moto. Akautia mikononi mwa yule mtu aliyevaa nguo ya kitani, naye alipoupokea, akatoka nje.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na kerubi yule akanyosha mkono wake toka katikati ya makerubi, kwa moto ule uliokuwa katikati ya makerubi, akatwaa baadhi ya moto ule, akautia katika mikono ya mtu yule aliyevaa bafta; naye akautwaa, akatoka.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kiumbe mmoja akanyosha mkono wake kuchukua moto uliokuwa katikati ya viumbe wenye mabawa, akatwaa sehemu yake na kuutia mikononi mwa yule mtu aliyevaa mavazi ya kitani; naye alipoupokea, akaenda zake.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Ndipo mmoja wa wale makerubi akanyoosha mkono wake kwenye moto uliokuwa katikati yao. Akachukua baadhi ya moto na kuutia mikononi mwa yule mtu aliyevaa mavazi ya kitani, naye akaupokea akatoka nje.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Ndipo mmoja wa wale makerubi akanyoosha mkono wake kwenye moto uliokuwa katikati yao. Akachukua baadhi ya moto na kuutia mikononi mwa yule mtu aliyevaa mavazi ya kitani, naye akaupokea akatoka nje.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na kerubi yule akanyosha mkono wake toka katikati ya makerubi, kwa moto ule uliokuwa katikati ya makerubi, akatwaa baadhi ya moto ule, akautia katika mikono ya mtu yule aliyevaa bafta; naye akautwaa, akatoka.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kiumbe mmoja akanyosha mkono wake kuchukua moto uliokuwa katikati ya viumbe wenye mabawa, akatwaa sehemu yake na kuutia mikononi mwa yule mtu aliyevaa mavazi ya kitani; naye alipoupokea, akaenda zake.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
ndipo, Kerubi alipokunjua mkono wake kwenye Makerubi na kuupeleka penye moto uliokuwa katikati ya Makerubi, akautwaa, akampa mwenye vazi la ukonge na kuutia katika viganja vyake, naye akauchukua, akatoka.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na kerubi yule akanyosha mkono wake toka katikati ya makerubi, kwa moto ule uliokuwa katikati ya makerubi, akatwaa baadhi ya moto ule, akautia katika mikono ya mtu yule aliyevaa bafta; naye akautwaa, akatoka.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kerubi mumoja akanyoosha mukono wake kwa kutwaa moto uliokuwa katikati ya makerubi, akatwaa sehemu yake na kuutia katika mikono ya yule mutu aliyevaa nguo ya kitani; naye alipoupokea, akajiendea.