Ezekiel 11:1 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Roho ya Mungu ikaninyanyua na kunipeleka mpaka lango la mashariki la nyumba ya Mwenyezi-Mungu. Huko nikawaona watu ishirini na watano wakiwamo Yaazania mwana wa Azuri na Pelatia mwana wa Benaya, ambao ni viongozi wa Waisraeli.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Ndipo Roho wa Mungu akaniinua na kunileta hadi kwenye lango la nyumba ya Mwenyezi Mungu linalotazama upande wa mashariki. Pale kwenye ingilio la lango palikuwa na wanaume ishirini na watano. Nami nikaona miongoni mwao Yaazania mwana wa Azuri na Pelatia mwana wa Benaya, viongozi wa watu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Tena roho ikaniinua, ikanileta hata lango la upande wa mashariki wa nyumba ya Bwana, lililoelekea upande wa mashariki; na tazama, mahali pa kuingilia pa lango walikuwako watu ishirini na watano; na katikati yao nikamwona Yaazania, mwana wa Azuri, na Pelatia, mwana wa Benaya, nao ni wakuu wa watu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Roho ya Mungu ikaninyanyua na kunipeleka mpaka lango la mashariki la nyumba ya Mwenyezi-Mungu. Huko nikawaona watu ishirini na watano wakiwamo Yaazania mwana wa Azuri na Pelatia mwana wa Benaya, ambao ni viongozi wa Waisraeli.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Ndipo Roho akaniinua na kunileta mpaka kwenye lango la nyumba ya BWANA linalotazama upande wa mashariki. Pale kwenye ingilio la lango kulikuwepo wanaume ishirini na watano, nami nikaona miongoni mwao Yaazania mwana wa Azuri na Pelatia mwana wa Benaya, viongozi wa watu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Ndipo Roho akaniinua na kunileta mpaka kwenye lango la nyumba ya bwana linalotazama upande wa mashariki. Pale kwenye ingilio la lango kulikuwepo wanaume ishirini na watano, nami nikaona miongoni mwao Yaazania mwana wa Azuri na Pelatia mwana wa Benaya, viongozi wa watu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Tena roho ikaniinua, ikanileta hadi katika lango la upande wa mashariki mwa nyumba ya BWANA, lililoelekea upande wa mashariki; na tazama, mahali pa kuingilia pa lango walikuwako watu ishirini na watano; na katikati yao nikamwona Yaazania, mwana wa Azuri, na Pelatia, mwana wa Benaya, nao ni wakuu wa watu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Roho ya Mungu ikaninyanyua na kunipeleka mpaka lango la mashariki la nyumba ya Mwenyezi-Mungu. Huko nikawaona watu ishirini na watano wakiwamo Yaazania mwana wa Azuri na Pelatia mwana wa Benaya, ambao ni viongozi wa Waisraeli.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Roho ikanichukua, ikanipeleka kwenye lango la Nyumba ya Bwana la mashariki lielekealo maawioni kwa jua. Hapo pa kulilingilia lile lango nikapaona waume 25; katikati yao nikamwona Yazania, mwana wa Azuri, na Pelatia, mwana wa Benaya, walio wakuu wa ukoo huu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Tena roho ikaniinua, ikanileta hata lango la upande wa mashariki wa nyumba ya BWANA, lililoelekea upande wa mashariki; na tazama, mahali pa kuingilia pa lango walikuwako watu ishirini na watano; na katikati yao nikamwona Yaazania, mwana wa Azuri, na Pelatia, mwana wa Benaya, nao ni wakuu wa watu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Roho wa Mungu akaninyanyua na kunipeleka mpaka kwenye mulango wa upande wa mashariki wa nyumba ya Yawe. Huko nikawaona watu makumi mbili na watano. Kati yao kulikuwa Yazania mwana wa Azuri na Pelatia mwana wa Benaya, ambao ni wakubwa wa Waisraeli.