Ezekiel 11:12 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Nanyi mtatambua kwamba mimi ni Mwenyezi-Mungu ambaye sheria zake hamkuzifuata na maagizo yake hamkutekeleza, bali mmetenda kulingana na maagizo ya mataifa yanayowazunguka.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Nanyi mtajua kuwa Mimi ndimi Mwenyezi Mungu, kwa kuwa hamkufuata amri zangu wala kuzishika sheria zangu, bali mmefuata mwenendo wa mataifa yanayowazunguka.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
nanyi mtajua ya kuwa mimi ni Bwana; kwa maana hamuendi katika amri zangu, wala hamkuzishika hukumu zangu, bali mmetenda mambo kama hukumu za mataifa wanaowazunguka.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Nanyi mtatambua kwamba mimi ni Mwenyezi-Mungu ambaye sheria zake hamkuzifuata na maagizo yake hamkutekeleza, bali mmetenda kulingana na maagizo ya mataifa yanayowazunguka.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Nanyi mtajua ya kuwa Mimi ndimi BWANA, kwa kuwa hamkufuata amri zangu wala kuzishika sheria zangu, bali mmefuata mwenendo wa mataifa yanayowazunguka.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Nanyi mtajua ya kuwa Mimi ndimi bwana, kwa kuwa hamkufuata amri zangu wala kuzishika sheria zangu, bali mmefuata mwenendo wa mataifa yanayowazunguka.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
nanyi mtajua ya kuwa mimi ni BWANA; kwa maana hamuendi katika amri zangu, wala hamkuzishika hukumu zangu, bali mmetenda mambo kama hukumu za mataifa wanaowazunguka.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Nanyi mtatambua kwamba mimi ni Mwenyezi-Mungu ambaye sheria zake hamkuzifuata na maagizo yake hamkutekeleza, bali mmetenda kulingana na maagizo ya mataifa yanayowazunguka.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ndipo, mtakapojua, ya kuwa mimi ni Bwana; hamkuyafuata maongozi yangu, wala hamkuyafanya mashauri yangu, ila mmefanya, kama wamizimu wawazungukao wanavyopiga mashauri.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
nanyi mtajua ya kuwa mimi ni BWANA; kwa maana hamuendi katika amri zangu, wala hamkuzishika hukumu zangu, bali mmetenda mambo kama hukumu za mataifa wanaowazunguka.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Nanyi mutatambua kwamba mimi ni Yawe ambaye hamukufuata masharti yake na maagizo yake hamukuyatimiza, lakini mumetenda kufuatana na maagizo ya mataifa yanayowazunguka.