Ezekiel 11:13 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Nilipokuwa natabiri, Pelatia mwana wa Benaya akafariki. Nami nikaanguka kifudifudi, nikalia kwa sauti kubwa, nikisema, “Ee Bwana Mwenyezi-Mungu, je, utawamaliza kabisa Waisraeli waliobaki?”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Basi nilipokuwa nikitoa unabii, Pelatia mwana wa Benaya akafa. Ndipo nikaanguka kifudifudi, nikalia kwa sauti kuu, nikasema, “Ee Bwana Mungu Mwenyezi! Je, utaangamiza kabisa mabaki ya Israeli?”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Ikawa, nilipotoa unabii, Pelatia, mwana wa Benaya, akafa. Ndipo nikaanguka kifudifudi, nikalia kwa sauti kuu, nikasema, Ee Bwana MUNGU, je! Utawakomesha kabisa mabaki ya Israeli?
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Nilipokuwa natabiri, Pelatia mwana wa Benaya akafariki. Nami nikaanguka kifudifudi, nikalia kwa sauti kubwa, nikisema, “Ee Bwana Mwenyezi-Mungu, je, utawamaliza kabisa Waisraeli waliobaki?”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Basi nilipokuwa ninatoa unabii, Pelatia mwana wa Benaya akafa. Ndipo nikaanguka kifudifudi, nikalia kwa sauti kuu nikasema, “Ee BWANA Mwenyezi! Je utaangamiza kabisa mabaki ya Israeli?”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Basi nilipokuwa ninatoa unabii, Pelatia mwana wa Benaya akafa. Ndipo nikaanguka kifudifudi, nikalia kwa sauti kuu nikasema, “Ee bwana Mwenyezi! Je utaangamiza kabisa mabaki ya Israeli?”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Ikawa, nilipotoa unabii, Pelatia, mwana wa Benaya, akafa. Ndipo nikaanguka kifudifudi, nikalia kwa sauti kuu, nikasema, Ee Bwana MUNGU, je! Utawakomesha kabisa mabaki ya Israeli?
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Nilipokuwa natabiri, Pelatia mwana wa Benaya akafariki. Nami nikaanguka kifudifudi, nikalia kwa sauti kubwa, nikisema, “Ee Bwana Mwenyezi-Mungu, je, utawamaliza kabisa Waisraeli waliobaki?”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ikawa, nilipowafumbulia haya, ndipo, Pelatia, mwana wa Benaya, alipokufa; nikaanguka kifudifudi na kulia kwa sauti kuu nikisema: E Bwana Mungu, wewe utalimaliza sao lake Isiraeli!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Ikawa, nilipotoa unabii, Pelatia, mwana wa Benaya, akafa. Ndipo nikaanguka kifudifudi, nikalia kwa sauti kuu, nikasema, Ee Bwana MUNGU, je! Utawakomesha kabisa mabaki ya Israeli?
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Nilipokuwa ninatabiri, Pelatia mwana wa Benaya akakufa. Nami nikaanguka uso mpaka chini, nikalia kwa sauti kubwa, nikisema: Ee Bwana Yawe, utawamaliza kabisa Waisraeli waliobaki?