Ezekiel 11:15 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
“Wewe mtu, ndugu zako na wakazi wa Yerusalemu ambao pia ni ndugu zako wanasema juu yako na juu ya watu wote wa Israeli walioko uhamishoni, ‘Nyinyi mlio uhamishoni mko mbali sana na Mwenyezi-Mungu; maana Mwenyezi-Mungu ametupa sisi nchi hii iwe mali yetu.’
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“Mwanadamu, ndugu zako, ndugu zako ambao ni wa uhusiano wa damu nawe pamoja na nyumba yote ya Israeli, ndio wale ambao watu wa Yerusalemu wamesema kuwahusu, ‘Wako mbali na Mwenyezi Mungu; nchi hii tulipewa sisi kuwa milki yetu.’
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Mwanadamu, ndugu zako, naam, ndugu zako, watu wa jamaa zako, na nyumba yote ya Israeli, wote pia, ndio hao ambao wenyeji wa Yerusalemu wamewaambia, Jitengeni mbali na Bwana, nchi hii tumepewa sisi, iwe milki yetu;
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
“Wewe mtu, ndugu zako na wakazi wa Yerusalemu ambao pia ni ndugu zako wanasema juu yako na juu ya watu wote wa Israeli walioko uhamishoni, ‘Nyinyi mlio uhamishoni mko mbali sana na Mwenyezi-Mungu; maana Mwenyezi-Mungu ametupa sisi nchi hii iwe mali yetu.’
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“Mwanadamu, ndugu zako, ndugu zako ambao ni wa uhusiano wa damu na nyumba yote ya Israeli, ndio wale ambao watu wa Yerusalemu wamesema, ‘Wako mbali na BWANA; nchi hii tulipewa sisi kuwa milki yetu.’
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“Mwanadamu, ndugu zako, ndugu zako ambao ni wa uhusiano wa damu na nyumba yote ya Israeli, ndio wale ambao watu wa Yerusalemu wamesema, ‘Wako mbali na bwana; nchi hii tulipewa sisi kuwa milki yetu.’
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Mwanadamu, ndugu zako, naam, ndugu zako, watu wa jamaa zako, na nyumba yote ya Israeli, wote pia, ndio hao ambao wenyeji wa Yerusalemu wamewaambia, Jitengeni mbali na BWANA, nchi hii tumepewa sisi, iwe milki yetu;
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
“Wewe mtu, ndugu zako na wakazi wa Yerusalemu ambao pia ni ndugu zako wanasema juu yako na juu ya watu wote wa Israeli walioko uhamishoni, ‘Nyinyi mlio uhamishoni mko mbali sana na Mwenyezi-Mungu; maana Mwenyezi-Mungu ametupa sisi nchi hii iwe mali yetu.’
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Mwana wa mtu, ndugu zako, hawa ndugu zako, ambao mlitekwa pamoja nao, hata mlango wote wa Isiraeli, hawa wote ndio, wenyeji wa Yerusalemu waliowaambia: Nendeni mbali mkitoka kwake Bwana! Sisi tumepewa nchi hii, iwe yetu!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Mwanadamu, ndugu zako, naam, ndugu zako, watu wa jamaa zako, na nyumba yote ya Israeli, wote pia, ndio hao ambao wenyeji wa Yerusalemu wamewaambia, Jitengeni mbali na BWANA, nchi hii tumepewa sisi, iwe milki yetu;
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Wewe mwanadamu, wandugu zako na wakaaji wa Yerusalema ambao vilevile ni wandugu zako wanasema juu yako na juu ya watu wote wa Israeli wanaokuwa katika uhamisho hivi: Ninyi munaokuwa katika uhamisho muko mbali sana na Yawe; maana Yawe ametupatia sisi inchi hii ikuwe mali yetu.