Ezekiel 11:17 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
“Basi, waambie kuwa mimi Bwana Mwenyezi-Mungu nasema hivi: Nitawakusanya toka miongoni mwa watu mnakokaa. Nitawakusanya kutoka nchi ambako mlitawanywa. Nitawarudisha nchini Israeli.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“Kwa hiyo sema: ‘Hili ndilo asemalo Bwana Mungu Mwenyezi: Nitawakusanya kutoka mataifa na kuwarudisha kutoka nchi ambazo mmetawanywa, nami nitawarudishia nchi ya Israeli.’
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Basi nena, Bwana MUNGU asema hivi; Nitawakusanya ninyi toka kati ya kabila za watu, na kuwakutanisha toka nchi zile mlizotawanyika, nami nitawapeni nchi ya Israeli.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
“Basi, waambie kuwa mimi Bwana Mwenyezi-Mungu nasema hivi: Nitawakusanya toka miongoni mwa watu mnakokaa. Nitawakusanya kutoka nchi ambako mlitawanywa. Nitawarudisha nchini Israeli.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“Kwa hiyo sema: ‘Hili ndilo BWANA Mwenyezi asemalo: Nitawakusanyeni kutoka katika mataifa na kuwarudisha kutoka katika nchi ambazo mmetawanywa, nami nitawarudishia nchi ya Israeli.’
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“Kwa hiyo sema: ‘Hili ndilo bwana Mwenyezi asemalo: Nitawakusanyeni kutoka mataifa na kuwarudisha kutoka nchi ambazo mmetawanywa, nami nitawarudishia nchi ya Israeli.’
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Basi nena, Bwana MUNGU asema hivi; Nitawakusanya ninyi toka kati ya makabila ya watu, na kuwakutanisha toka nchi zile mlizotawanyika, nami nitawapeni nchi ya Israeli.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
“Basi, waambie kuwa mimi Bwana Mwenyezi-Mungu nasema hivi: Nitawakusanya toka miongoni mwa watu mnakokaa. Nitawakusanya kutoka nchi ambako mlitawanywa. Nitawarudisha nchini Israeli.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kwa hiyo sema: Hivi ndivyo Bwana Mungu anavyosema: Nitawakusanya ninyi na kuwatoa katika hayo makabila, kweli nitawaunganisha ninyi na kuwatoa katika nchi hizo, nilikowatawanya, niwape ninyi nchi ya Isiraeli.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Basi nena, Bwana MUNGU asema hivi; Nitawakusanya ninyi toka kati ya kabila za watu, na kuwakutanisha toka nchi zile mlizotawanyika, nami nitawapeni nchi ya Israeli.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Basi, Bwana wetu Yawe anasema hivi: Nitawakusanya toka kati ya watu, nitawakusanya kutoka katika inchi ambako mulisambazwa. Nitawarudisha katika inchi ya Israeli.