Ezekiel 11:19 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Nitawapeni moyo mpya na kuweka roho mpya ndani yenu. Nitauondoa ule moyo mgumu kama jiwe na kuwapa moyo wa utii,
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Nitawapa moyo usiogawanyika na kuweka roho mpya ndani yao; nitaondoa ndani yao moyo wa jiwe na kuwapa moyo wa nyama.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Nami nitawapa moyo mmoja, nami nitatia roho mpya ndani yao; nami nitauondoa moyo wa kijiwe katika miili yao, nami nitawapa moyo wa nyama;
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Nitawapeni moyo mpya na kuweka roho mpya ndani yenu. Nitauondoa ule moyo mgumu kama jiwe na kuwapa moyo wa utii,
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Nitawapa moyo mmoja na kuweka roho mpya ndani yao, nitaondoa kutoka ndani yao moyo wa jiwe na kuwapa moyo wa nyama.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Nitawapa moyo mmoja na kuweka roho mpya ndani yao, nitaondoa kutoka ndani yao moyo wa jiwe na kuwapa moyo wa nyama.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Nami nitawapa moyo mmoja, nami nitatia roho mpya ndani yao; nami nitauondoa moyo wa jiwe katika miili yao, nami nitawapa moyo wa nyama;
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Nitawapeni moyo mpya na kuweka roho mpya ndani yenu. Nitauondoa ule moyo mgumu kama jiwe na kuwapa moyo wa utii,
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Nami nitawapa kuwa moyo mmoja, tena nitatia roho moja mioyoni mwao; namo miilini mwao nitaitoa mioyo iliyo migumu kama mawe nikiwatia mioyo inayolegea kama nyama.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Nami nitawapa moyo mmoja, nami nitatia roho mpya ndani yao; nami nitauondoa moyo wa kijiwe katika miili yao, nami nitawapa moyo wa nyama;
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Nitawapa moyo mupya na kuweka roho mupya ndani yenu. Nitauondoa ule moyo mugumu kama jiwe na kuwapa moyo musikilivu,