Ezekiel 12:13 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Lakini nitatandaza wavu wangu juu yake, naye atanaswa katika mtego wangu. Nitampeleka Babuloni, nchi ya Wakaldayo; naye akiwa huko atakufa bila kuiona hiyo nchi.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Nitamtandazia wavu wangu, naye atanaswa kwenye mtego wangu; nitamleta hadi Babeli, nchi ya Wakaldayo, lakini hataiona, naye atafia huko.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Tena wavu wangu nitautandika juu yake, naye atanaswa kwa mtego wangu; nami nitampeleka Babeli, mpaka nchi ya Wakaldayo; lakini hataiona, angawa atakufa huko.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Lakini nitatandaza wavu wangu juu yake, naye atanaswa katika mtego wangu. Nitampeleka Babuloni, nchi ya Wakaldayo; naye akiwa huko atakufa bila kuiona hiyo nchi.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Nitatandaza wavu wangu kwa ajili yake, naye atanaswa kwenye mtego wangu, nitamleta mpaka Babeli, nchi ya Wakaldayo, lakini hataiona, naye atafia huko.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Nitatandaza wavu wangu kwa ajili yake, naye atanaswa kwenye mtego wangu, nitamleta mpaka Babeli, nchi ya Wakaldayo, lakini hataiona, naye atafia huko.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Tena wavu wangu nitautandika juu yake, naye atanaswa kwa mtego wangu; nami nitampeleka Babeli, mpaka nchi ya Wakaldayo; bali hataiona, ingawa atakufa huko.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Lakini nitatandaza wavu wangu juu yake, naye atanaswa katika mtego wangu. Nitampeleka Babuloni, nchi ya Wakaldayo; naye akiwa huko atakufa bila kuiona hiyo nchi.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Nami nitamtegea wavu wangu, anaswe katika tanzi langu; kisha nitampeleka Babeli katika nchi ya Wakasidi, lakini hataiona; nako ndiko, atakakokufa.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Tena wavu wangu nitautandika juu yake, naye atanaswa kwa mtego wangu; nami nitampeleka Babeli, mpaka nchi ya Wakaldayo; lakini hataiona, angawa atakufa huko.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Lakini nitatandaza wavu wangu juu yake, naye atanaswa katika mutego wangu. Nitamupeleka Babeli, inchi ya Wakaldea; naye akiwa huko atakufa bila kuiona inchi hiyo.