Ezekiel 12:19 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Waambie watu wa nchi hii, kuwa mimi Bwana Mwenyezi-Mungu nasema juu ya wakazi wa Yerusalemu ambao bado wamo nchini Israeli, kwamba watakula chakula chao kwa hofu na watakunywa maji yao kwa kufadhaika, kwani nchi yao haitakuwa na kitu, kwa sababu kila mkazi ni mdhalimu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Waambie watu wa nchi: ‘Hili ndilo asemalo Bwana Mungu Mwenyezi kuhusu wakaaji wa Yerusalemu na katika nchi ya Israeli: Watakula chakula chao kwa wasiwasi na kunywa maji yao kwa kufadhaika, kwa kuwa nchi yao itanyang’anywa kila kitu chake kwa sababu ya udhalimu wa wote wanaoishi humo.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
ukawaambie watu wa nchi, Bwana MUNGU asema hivi, katika habari zao wakaao Yerusalemu, na katika nchi ya Israeli; Watakula chakula chao kwa kukitunza sana, na maji yao watayanywa kwa ushangao, nchi yao iwe ukiwa, kwa kukosa vitu vyote viijazavyo, kwa sababu ya udhalimu wao wote wakaao ndani yake.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Waambie watu wa nchi hii, kuwa mimi Bwana Mwenyezi-Mungu nasema juu ya wakazi wa Yerusalemu ambao bado wamo nchini Israeli, kwamba watakula chakula chao kwa hofu na watakunywa maji yao kwa kufadhaika, kwani nchi yao haitakuwa na kitu, kwa sababu kila mkazi ni mdhalimu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Waambie watu wa nchi: ‘Hili ndilo BWANA Mwenyezi asemalo kuhusu hao wanaoishi Yerusalemu na katika nchi ya Israeli: Watakula chakula chao kwa wasiwasi na kunywa maji yao kwa kufadhaika, kwa kuwa nchi yao itanyang'anywa kila kitu chake kwa sababu ya udhalimu wa wote wanaoishi humo.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Waambie watu wa nchi: ‘Hili ndilo bwana Mwenyezi asemalo kuhusu hao wanaoishi Yerusalemu na katika nchi ya Israeli: Watakula chakula chao kwa wasiwasi na kunywa maji yao kwa kufadhaika, kwa kuwa nchi yao itanyang’anywa kila kitu chake kwa sababu ya udhalimu wa wote wanaoishi humo.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
ukawaambie watu wa nchi, Bwana MUNGU asema hivi, kuhusu habari zao wakaao Yerusalemu, na katika nchi ya Israeli; Watakula chakula chao kwa kukitunza sana, na maji yao watayanywa kwa ushangao, nchi yao iwe ukiwa, kwa kukosa vitu vyote viijazavyo, kwa sababu ya udhalimu wao wote wakaao ndani yake.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Waambie watu wa nchi hii, kuwa mimi Bwana Mwenyezi-Mungu nasema juu ya wakazi wa Yerusalemu ambao bado wamo nchini Israeli, kwamba watakula chakula chao kwa hofu na watakunywa maji yao kwa kufadhaika, kwani nchi yao haitakuwa na kitu, kwa sababu kila mkazi ni mdhalimu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kisha waambie watu wa nchi hii: Hivi ndivyo, Bwana Mungu anavyowaambia wakaao Yerusalemu katika nchi ya Isiraeli: Vyakula vyenu mtavila na kuvihangaikia, nayo maji yenu mtayanywa kwa kupigwa na bumbuazi, kwani nchi yao itaangamia, yote yaliyojaa mle yakipotea kwa ajili ya ukorofi wao wote waliokaa huko.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
ukawaambie watu wa nchi, Bwana MUNGU asema hivi, katika habari zao wakaao Yerusalemu, na katika nchi ya Israeli; Watakula chakula chao kwa kukitunza sana, na maji yao watayanywa kwa ushangao, nchi yao iwe ukiwa, kwa kukosa vitu vyote viijazavyo, kwa sababu ya udhalimu wao wote wakaao ndani yake.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Uwaambie watu wa inchi hii: Bwana wetu Yawe anasema hivi juu ya wakaaji wa Yerusalema ambao wangali bado katika inchi ya Waisraeli: Watakula chakula chao kwa hofu na kunywa maji yao kwa kufazaika, maana inchi yao haitakuwa na kitu, kwa sababu kila mukaaji ni mutesaji mukali.