Ezekiel 12:23 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Waambie kuwa mimi Bwana Mwenyezi-Mungu nasema kwamba nitakomesha methali hiyo nao hawataitumia tena nchini Israeli. Waambie kuwa wakati umewadia ambapo maono yote yatatimia.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Waambie, ‘Hili ndilo asemalo Bwana Mungu Mwenyezi: Nitaikomesha mithali hii, nao hawataitumia tena katika Israeli.’ Waambie, ‘Siku zimekaribia ambapo kila ono litatimizwa.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Basi uwaambie, Bwana MUNGU asema hivi; Nitaikomesha mithali hii, wasiitumie tena kama mithali katika Israeli; lakini uwaambie, Siku hizo ni karibu, na utimilizo wa maono yote.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Waambie kuwa mimi Bwana Mwenyezi-Mungu nasema kwamba nitakomesha methali hiyo nao hawataitumia tena nchini Israeli. Waambie kuwa wakati umewadia ambapo maono yote yatatimia.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Waambie, ‘Hili ndilo BWANA Mwenyezi asemalo: Nitaikomesha mithali hii, nao hawataitumia tena katika Israeli.’ Waambie, ‘Siku zimekaribia wakati kila maono yatakapotimizwa.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Waambie, ‘Hili ndilo bwana Mwenyezi asemalo: Nitaikomesha mithali hii, nao hawataitumia tena katika Israeli.’ Waambie, ‘Siku zimekaribia wakati kila maono yatakapotimizwa.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Basi uwaambie, Bwana MUNGU asema hivi; Nitaikomesha mithali hii, wasiitumie tena kama mithali katika Israeli; lakini uwaambie, Siku hizo ni karibu, na utimilizo wa maono yote.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Waambie kuwa mimi Bwana Mwenyezi-Mungu nasema kwamba nitakomesha methali hiyo nao hawataitumia tena nchini Israeli. Waambie kuwa wakati umewadia ambapo maono yote yatatimia.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kwa hiyo waambie: Hivi ndivyo, Bwana Mungu anavyosema: Nitalikomesha fumbo hilo, wasilitumie tena kwao Waisiraeli; kwa hiyo waambie: Siku hizo ziko karibu kweli, maono yote yatimie.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Basi uwaambie, Bwana MUNGU asema hivi; Nitaikomesha mithali hii, wasiitumie tena kama mithali katika Israeli; lakini uwaambie, Siku hizo ni karibu, na utimilizo wa maono yote.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Uwaambie kwamba Bwana wetu Yawe anasema kwamba nitakomesha mezali hiyo nao hawataitumia tena katika inchi ya Waisraeli. Uwaambie kwamba wakati umefika ambapo maono yote yatatimia.