Ezekiel 13:14 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Nitaubomolea mbali huo ukuta mlioupaka chokaa, na msingi wake utakuwa wazi. Ukuta huo ukianguka, mtaangamia chini yake. Ndipo mtakapotambua mimi ni Mwenyezi-Mungu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Nitaubomoa ukuta mlioupaka chokaa na kuuangusha chini ili msingi wake uwe wazi. Utakapoanguka, mtaangamizwa ndani yake, nanyi mtajua kuwa Mimi ndimi Mwenyezi Mungu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Ndivyo nitakavyoubomoa ukuta mlioupaka chokaa isiyokorogwa vema, na kuuangusha chini, hata misingi yake itafunuliwa; nao utaanguka, nanyi mtaangamizwa katikati yake; nanyi mtajua ya kuwa mimi ndimi Bwana.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Nitaubomolea mbali huo ukuta mlioupaka chokaa, na msingi wake utakuwa wazi. Ukuta huo ukianguka, mtaangamia chini yake. Ndipo mtakapotambua mimi ni Mwenyezi-Mungu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Nitaubomoa ukuta mlioupaka chokaa na kuuangusha chini ili msingi wake uachwe wazi. Utakapoanguka, mtaangamizwa ndani yake, nanyi mtajua kuwa Mimi ndimi BWANA.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Nitaubomoa ukuta mlioupaka chokaa na kuuangusha chini ili msingi wake uachwe wazi. Utakapoanguka, mtaangamizwa ndani yake, nanyi mtajua kuwa Mimi ndimi bwana.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Ndivyo nitakavyoubomoa ukuta mlioupaka chokaa isiyokorogwa vema, na kuuangusha chini, hata misingi yake itafunuliwa; nao utaanguka, nanyi mtaangamizwa katikati yake; nanyi mtajua ya kuwa mimi ndimi BWANA.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Nitaubomolea mbali huo ukuta mlioupaka chokaa, na msingi wake utakuwa wazi. Ukuta huo ukianguka, mtaangamia chini yake. Ndipo mtakapotambua mimi ni Mwenyezi-Mungu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ndipo, nitakapolibomoa boma, mlilolipaka chokaa, nitaliangusha chini, msingi wake utokee; napo, litakapoanguka, mtaangamia huko katikati. Ndipo, mtakapojua, ya kuwa mimi ni Bwana.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Ndivyo nitakavyoubomoa ukuta mlioupaka chokaa isiyokorogwa vema, na kuuangusha chini, hata misingi yake itafunuliwa; nao utaanguka, nanyi mtaangamizwa katikati yake; nanyi mtajua ya kuwa mimi ndimi BWANA.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Nitaubomoa kabisa huo ukuta mulioupakaa chokaa, na musingi wake utakuwa wazi. Ukuta huo ukianguka, mutaangamia chini yake. Halafu mutatambua kwamba mimi ni Yawe.