Ezekiel 13:18 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
na kuwaambia kuwa Bwana Mwenyezi-Mungu asema hivi: Ole wenu wanawake mnaoshona tepe za hirizi za kuvaa mikononi mwa kila mtu na kutengeneza shela zenye hirizi za kila kimo ili kuyawinda maisha ya watu. Je, mnapowinda maisha ya watu wangu mnadhani mtasalimisha maisha yenu wenyewe?
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
na useme, ‘Hili ndilo asemalo Bwana Mungu Mwenyezi: Ole wao wanawake washonao hirizi za uchawi juu ya viwiko vyao vyote na kutengeneza shela za urefu wa aina mbalimbali kwa ajili ya kufunika vichwa vyao kwa makusudi ya kuwanasa watu. Je, mtatega uhai wa watu wangu lakini ninyi mponye wa kwenu?
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
useme, Bwana MUNGU asema hivi; Ole wao wanawake wale, washonao hirizi katika viungo vyote vya mikono, wawekao leso juu ya vichwa vya kila kimo, ili wawinde roho za watu; je! Mtaziwinda roho za watu wangu, na kuzihifadhi hai roho zenu wenyewe?
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
na kuwaambia kuwa Bwana Mwenyezi-Mungu asema hivi: Ole wenu wanawake mnaoshona tepe za hirizi za kuvaa mikononi mwa kila mtu na kutengeneza shela zenye hirizi za kila kimo ili kuyawinda maisha ya watu. Je, mnapowinda maisha ya watu wangu mnadhani mtasalimisha maisha yenu wenyewe?
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
na useme, ‘Hili ndilo BWANA Mwenyezi asemalo: Ole wao wanawake washonao hirizi za uchawi juu ya viwiko vyao vyote na kutengeneza shela za urefu wa aina mbalimbali kwa ajili ya kufunika vichwa vyao kwa makusudi ya kuwanasa watu. Je, mtatega uhai wa watu wangu lakini ninyi mponye wa kwenu?
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
na useme, ‘Hili ndilo bwana Mwenyezi asemalo: Ole wao wanawake washonao hirizi za uchawi juu ya viwiko vyao vyote na kutengeneza shela za urefu wa aina mbalimbali kwa ajili ya kufunika vichwa vyao kwa makusudi ya kuwanasa watu. Je, mtatega uhai wa watu wangu lakini ninyi mponye wa kwenu?
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
useme, Bwana MUNGU asema hivi; Ole wao wanawake wale, washonao hirizi katika viungo vyote vya mikono, wawekao leso juu ya vichwa vya kila kimo, ili wawinde roho za watu; je! Mtaziwinda roho za watu wangu, na kuzihifadhi hai roho zenu wenyewe?
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
na kuwaambia kuwa Bwana Mwenyezi-Mungu asema hivi: Ole wenu wanawake mnaoshona tepe za hirizi za kuvaa mikononi mwa kila mtu na kutengeneza shela zenye hirizi za kila kimo ili kuyawinda maisha ya watu. Je, mnapowinda maisha ya watu wangu mnadhani mtasalimisha maisha yenu wenyewe?
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Sema: Hivi ndivyo, Bwana Mungu anavyosema: Watapatwa na mambo hao wanawake wanaoshona vitambaa vya uganga katika maungo yote ya mikono, wanaotengeneza hata miharuma ilinganayo na vichwa vya kila umbo, kusudi wapate kunasa roho za watu! Je? Mwataka kuzinasa roho zao walio ukoo wangu, mziokoe roho zenu wenyewe?
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
useme, Bwana MUNGU asema hivi; Ole wao wanawake wale, washonao hirizi katika viungo vyote vya mikono, wawekao leso juu ya vichwa vya kila kimo, ili wawinde roho za watu; je! Mtaziwinda roho za watu wangu, na kuzihifadhi hai roho zenu wenyewe?
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
na kuwaambia kwamba Bwana wetu Yawe anasema hivi: Ole kwenu ninyi wanawake munaoshona vitepe vyenye hirizi ambavyo kila mutu anavivaa kwenye maunganio ya mikono na kutengeneza vitambaa vyenye hirizi za kila kimo kwa ajili ya watu wa kila umri. Munapowinda maisha ya watu wangu munazani kwamba mutaokoa maisha yenu wenyewe?