Ezekiel 13:19 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mmenikufuru mbele ya watu wangu ili kupata konzi za shayiri na chakula kidogo. Mnawaua watu wasiostahili kufa na kuwaacha hai wanaostahili kuuawa, kwa uongo wenu mnaowaambia watu wangu, nao wanawaamini.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Ninyi mmeninajisi miongoni mwa watu wangu kwa ajili ya konzi chache za shayiri na chembe za mkate. Kwa kuwanenea uongo watu wangu, ambao husikiliza uongo, mmewaua watu ambao hawakustahili kufa, na kuwaacha hai wale ambao walistahili kufa.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Nanyi mmeninajisi kati ya watu wangu, kwa ajili ya makonzi ya shayiri na vipande vya mkate, ili kuziua roho za watu ambao haiwapasi kufa, na kuzihifadhi hai roho za watu ambao haikuwapasa kuwa hai, kwa kuwaambia uongo watu wangu wasikilizao uongo.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mmenikufuru mbele ya watu wangu ili kupata konzi za shayiri na chakula kidogo. Mnawaua watu wasiostahili kufa na kuwaacha hai wanaostahili kuuawa, kwa uongo wenu mnaowaambia watu wangu, nao wanawaamini.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Ninyi mmeninajisi miongoni mwa watu wangu kwa ajili ya konzi chache za shayiri na chembe za mkate. Kwa kuwaambia uongo watu wangu, wale ambao husikiliza uongo, mmewaua wale watu ambao wasingekufa na kuwaacha hai wale ambao wasingeishi.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Ninyi mmeninajisi miongoni mwa watu wangu kwa ajili ya konzi chache za shayiri na chembe za mkate. Kwa kuwaambia uongo watu wangu, wale ambao husikiliza uongo, mmewaua wale watu ambao wasingekufa na kuwaacha hai wale ambao wasingeishi.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Nanyi mmeninajisi kati ya watu wangu, kwa ajili ya makonzi ya shayiri na vipande vya mkate, ili kuziua roho za watu ambao haiwapasi kufa, na kuzihifadhi hai roho za watu ambao haikuwapasa kuwa hai, kwa kuwaambia uongo watu wangu wasikilizao uongo.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mmenikufuru mbele ya watu wangu ili kupata konzi za shayiri na chakula kidogo. Mnawaua watu wasiostahili kufa na kuwaacha hai wanaostahili kuuawa, kwa uongo wenu mnaowaambia watu wangu, nao wanawaamini.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Mkanitia uchafu mbele yao walio wa ukoo wangu mkiweza kupata makufi mawili tu ya mawele au vipande vichache vya mkate; ndivyo, mnavyoziua roho za watu wasioipaswa na kufa, nazo roho za wengine wasiopaswa na kupona mnaziponya, mkiwaogopea walio ukoo wangu, wanaopenda kusikia maneno ya uwongo.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Nanyi mmeninajisi kati ya watu wangu, kwa ajili ya makonzi ya shayiri na vipande vya mkate, ili kuziua roho za watu ambao haiwapasi kufa, na kuzihifadhi hai roho za watu ambao haikuwapasa kuwa hai, kwa kuwaambia uongo watu wangu wasikilizao uongo.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Mumenizaraulisha mbele ya watu wangu kusudi mupate vitanga vya shayiri na chakula kidogo. Munawaua watu wasiostahili kufa na kuwaacha wazima wanaostahili kuuawa, kwa uongo wenu munaowaambia watu wangu, nao wanawaaminia.