Ezekiel 13:20 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
“Basi, mimi Bwana Mwenyezi-Mungu nasema: Nitashambulia hirizi zenu mnazowafunga nazo watu; nitazipasuapasua kutoka mikononi mwenu na kuwaacha huru hao mnaowawinda kama ndege.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“ ‘Kwa hiyo hili ndilo asemalo Bwana Mungu Mwenyezi: Niko kinyume na hizo hirizi zenu za uchawi mnazotumia kuwatega watu kama ndege, nami nitazirarua mikononi mwenu; nitawaweka huru watu mliowatega kama ndege.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Basi Bwana MUNGU asema hivi; Tazama, mimi ni kinyume cha hirizi zenu, ambazo kwa hizo mnaziwinda roho za watu kama ndege, nami nitazitoa katika mikono yenu kwa nguvu; nami nitaziachilia roho zile mnazoziwinda kama ndege.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
“Basi, mimi Bwana Mwenyezi-Mungu nasema: Nitashambulia hirizi zenu mnazowafunga nazo watu; nitazipasuapasua kutoka mikononi mwenu na kuwaacha huru hao mnaowawinda kama ndege.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“ ‘Kwa hiyo hili ndilo BWANA Mwenyezi asemalo: Mimi niko kinyume na hizo hirizi zenu za uchawi ambazo kwa hizo mnawatega watu kama ndege, nami nitazirarua kutoka mikononi mwenu, nitawaweka huru watu wale mliowatega kama ndege.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“ ‘Kwa hiyo hili ndilo bwana Mwenyezi asemalo: Mimi niko kinyume na hizo hirizi zenu za uchawi ambazo kwa hizo mnawatega watu kama ndege, nami nitazirarua kutoka mikononi mwenu, nitawaweka huru watu wale mliowatega kama ndege.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Basi Bwana MUNGU asema hivi; Tazama, mimi nazipinga hirizi zenu, ambazo kwa hizo mnaziwinda roho za watu kama ndege, nami nitazitoa katika mikono yenu kwa nguvu; nami nitaziachilia roho zile mnazoziwinda kama ndege.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
“Basi, mimi Bwana Mwenyezi-Mungu nasema: Nitashambulia hirizi zenu mnazowafunga nazo watu; nitazipasuapasua kutoka mikononi mwenu na kuwaacha huru hao mnaowawinda kama ndege.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kweli hivi ndivyo, Bwana Mungu anavyosema: Mtaniona, nikivijia vitambaa vyenu vya uganga, mnavyovitumia vya kunasia roho za watu, kama ni ndege, nitavirarua mikononi mwenu, nizinasue zile roho za watu kwenda zao, ni zile roho, mlizozinasa, kama ni ndege.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Basi Bwana MUNGU asema hivi; Tazama, mimi ni kinyume cha hirizi zenu, ambazo kwa hizo mnaziwinda roho za watu kama ndege, nami nitazitoa katika mikono yenu kwa nguvu; nami nitaziachilia roho zile mnazoziwinda kama ndege.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Basi, Bwana wetu Yawe anasema hivi: Nitashambulia hirizi zenu munazowafunga nazo watu; nitazipasuapasua toka katika mikono yenu na kuwaacha huru hao munaowawinda kama ndege.