Ezekiel 13:6 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Maono yao ni ya uongo mtupu na wanachotabiri ni udanganyifu mtupu. Hudai kwamba wanasema kwa niaba yangu mimi Mwenyezi-Mungu, lakini mimi sikuwatuma; kisha wananitazamia nitimize wanayosema.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Maono yao ni ya uongo na ubashiri wao ni wa udanganyifu. Wao husema, “Mwenyezi Mungu amesema”, wakati Mwenyezi Mungu hakuwatuma; bado wakitarajia maneno yao kutimizwa.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Wameona ubatili, na uganga wa uongo, hao wasemao, Bwana asema; lakini Bwana hakuwatuma; nao wamewatumainisha watu ya kuwa neno lile litatimizwa.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Maono yao ni ya uongo mtupu na wanachotabiri ni udanganyifu mtupu. Hudai kwamba wanasema kwa niaba yangu mimi Mwenyezi-Mungu, lakini mimi sikuwatuma; kisha wananitazamia nitimize wanayosema.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Maono yao ni ya uongo na ubashiri wao ni wa udanganyifu. Wao husema, “BWANA amesema,” wakati BWANA hakuwatuma, bado wakitarajia maneno yao kutimizwa.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Maono yao ni ya uongo na ubashiri wao ni wa udanganyifu. Wao husema, “ bwana amesema,” wakati bwana hakuwatuma, bado wakitarajia maneno yao kutimizwa.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Wameona ubatili, na uganga wa uongo, hao wasemao, BWANA asema; lakini BWANA hakuwatuma; nao wamewapa watu tumaini ya kuwa neno lile litatimizwa.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Maono yao ni ya uongo mtupu na wanachotabiri ni udanganyifu mtupu. Hudai kwamba wanasema kwa niaba yangu mimi Mwenyezi-Mungu, lakini mimi sikuwatuma; kisha wananitazamia nitimize wanayosema.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Wameona maono yasiyokuwako, nayo maaguo yao ni ya uwongo, wakisema: Ndivyo, asemavyo Bwana, lakini Bwana hakuwatuma, nao wakangojea, alitimize neno lao.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Wameona ubatili, na uganga wa uongo, hao wasemao, BWANA asema; lakini BWANA hakuwatuma; nao wamewatumainisha watu ya kuwa neno lile litatimizwa.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Maono yao ni ya uongo mutupu na wanachotabiri ni udanganyifu mutupu. Wanasema “Ni ujumbe wa Yawe” lakini Yawe hakuwatuma; kisha wanamutazamia atimize yale wanayosema.