Ezekiel 13:7 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Basi, nawaulizeni: Je, maono yenu si uongo mtupu na utabiri wenu udanganyifu? Nyinyi mnadai kwamba mnasema kwa jina langu hali mimi sijaongea nanyi kamwe!
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Je, hamjaona maono ya uongo na kusema ubashiri wa udanganyifu, hapo msemapo, “Mwenyezi Mungu asema”, wakati Mimi sijasema?
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Je! Hamkuona maono ya bure, hamkunena mabashiri ya uongo? Nanyi mwasema, Bwana asema; ila mimi sikusema neno.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Basi, nawaulizeni: Je, maono yenu si uongo mtupu na utabiri wenu udanganyifu? Nyinyi mnadai kwamba mnasema kwa jina langu hali mimi sijaongea nanyi kamwe!
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Je, hamjaona maono ya uongo na kusema ubashiri wa udanganyifu hapo msemapo, “BWANA asema,” lakini Mimi sijasema?
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Je, hamjaona maono ya uongo na kusema ubashiri wa udanganyifu hapo msemapo, “ bwana asema,” lakini Mimi sijasema?
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Je! Hamkuona maono ya bure, hamkunena ubashiri wa uongo? Nanyi mwasema, BWANA asema; ila mimi sikusema neno.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Basi, nawaulizeni: Je, maono yenu si uongo mtupu na utabiri wenu udanganyifu? Nyinyi mnadai kwamba mnasema kwa jina langu hali mimi sijaongea nanyi kamwe!
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Je? Hamkuona maono yasiyokuwako? Hamkusema maaguo ya uwongo, mliposema: Ndivyo, asemavyo Bwana, nami nalikuwa sikuyasema?
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Je! Hamkuona maono ya bure, hamkunena mabashiri ya uongo? Nanyi mwasema, BWANA asema; ila mimi sikusema neno.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Basi, ninawauliza: Maono yenu si uongo mutupu na utabiri wenu udanganyifu wakati munaposema “Ni ujumbe wa Yawe”, ijapokuwa mimi sijaongea nanyi hata kidogo?