Ezekiel 13:9 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Nitanyosha mkono wangu dhidi yenu nyinyi manabii mnaotoa maono ya uongo na kutabiri udanganyifu mtupu. Watu wangu watakapokutanika kuamua mambo, nyinyi hamtakuwapo. Wala hamtakuwa katika orodha ya watu wa Israeli na hamtaingia katika nchi ya Israeli; ndipo mtakapotambua kuwa mimi ni Bwana Mwenyezi-Mungu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Mkono wangu utakuwa dhidi ya manabii ambao huona maono ya uongo na kusema ubashiri wa udanganyifu. Hawatakuwa katika baraza la watu wangu au kuorodheshwa katika kumbukumbu ya nyumba ya Israeli, wala hawataingia katika nchi ya Israeli. Ndipo mtajua kuwa Mimi ndimi Bwana Mungu Mwenyezi.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na mkono wangu utakuwa juu ya manabii wanaoona ubatili, na kutabiri uongo; hawatakuwa katika mashauri ya watu wangu, wala hawataandikwa katika maandiko ya nyumba ya Israeli, wala hawataingia katika nchi ya Israeli; nanyi mtajua ya kuwa mimi ndimi Bwana MUNGU.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Nitanyosha mkono wangu dhidi yenu nyinyi manabii mnaotoa maono ya uongo na kutabiri udanganyifu mtupu. Watu wangu watakapokutanika kuamua mambo, nyinyi hamtakuwapo. Wala hamtakuwa katika orodha ya watu wa Israeli na hamtaingia katika nchi ya Israeli; ndipo mtakapotambua kuwa mimi ni Bwana Mwenyezi-Mungu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Mkono wangu utakuwa dhidi ya manabii ambao huona maono ya uongo na kusema ubashiri wa udanganyifu. Hawatakuwa katika baraza la watu wangu au kuandikwa katika kumbukumbu ya nyumba ya Israeli wala hawataingia katika nchi ya Israeli. Ndipo mtajua kuwa Mimi ndimi BWANA Mwenyezi.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Mkono wangu utakuwa dhidi ya manabii ambao huona maono ya uongo na kusema ubashiri wa udanganyifu. Hawatakuwa katika baraza la watu wangu au kuandikwa katika kumbukumbu ya nyumba ya Israeli wala hawataingia katika nchi ya Israeli. Ndipo mtajua kuwa Mimi ndimi bwana Mwenyezi.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na mkono wangu utakuwa juu ya manabii wanaoona ubatili, na kutabiri uongo; hawatakuwa katika mashauri ya watu wangu, wala hawataandikwa katika maandiko ya nyumba ya Israeli, wala hawataingia katika nchi ya Israeli; nanyi mtajua ya kuwa mimi ndimi Bwana MUNGU.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Nitanyosha mkono wangu dhidi yenu nyinyi manabii mnaotoa maono ya uongo na kutabiri udanganyifu mtupu. Watu wangu watakapokutanika kuamua mambo, nyinyi hamtakuwapo. Wala hamtakuwa katika orodha ya watu wa Israeli na hamtaingia katika nchi ya Israeli; ndipo mtakapotambua kuwa mimi ni Bwana Mwenyezi-Mungu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Itakuwa, mkono wangu uwajie hao wafumbuaji walioona yasiyokuwako na kuagua uwongo; hawatakula bia nao walio ukoo wangu, wala hawataandikwa katika kitabu cha mlango wa Isiraeli, wala hawataiingia nchi ya Isiraeli; ndipo, watakapojua, ya kuwa mimi ni Bwana Mungu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na mkono wangu utakuwa juu ya manabii wanaoona ubatili, na kutabiri uongo; hawatakuwa katika mashauri ya watu wangu, wala hawataandikwa katika maandiko ya nyumba ya Israeli, wala hawataingia katika nchi ya Israeli; nanyi mtajua ya kuwa mimi ndimi Bwana MUNGU.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Nitanyoosha mukono wangu juu yenu ninyi manabii munaotoa maono ya uongo na kutabiri udanganyifu mutupu. Watu wangu watakapokutanika kwa kuamua maneno, ninyi hamutakuwa pale. Wala hamutakuwa katika kitabu cha majina ya Waisraeli na hamutaingia katika inchi ya Waisraeli; halafu mutatambua kwamba mimi ni Bwana wenu Yawe.