Ezekiel 14:15 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Tena nitapeleka wanyama wa porini katika nchi hiyo na kuwanyanganya watoto wao na kuifanya nchi hiyo kuwa ukiwa, hata hakuna mtu yeyote atakayeweza kupita nchini humo kwa sababu ya wanyama wakali.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“Au nikiwaachilia wanyama pori katika nchi hiyo nao wakaiacha bila watoto, nayo ikawa ukiwa hivi kwamba hakuna mtu apitaye kwa sababu ya wanyama pori,
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Nikipitisha wanyama wabaya ndani ya nchi ile, wakaiharibu hata ikawa ukiwa, mtu awaye yote asiweze kupita ndani yake, kwa sababu ya wanyama hao;
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Tena nitapeleka wanyama wa porini katika nchi hiyo na kuwanyang'anya watoto wao na kuifanya nchi hiyo kuwa ukiwa, hata hakuna mtu yeyote atakayeweza kupita nchini humo kwa sababu ya wanyama wakali.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“Au kama nikipeleka wanyama pori katika nchi hiyo yote na kuifanya isiwe na watoto, nayo ikawa ukiwa kwamba hakuna mtu apitaye katika nchi hiyo kwa sababu ya wanyama pori,
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“Au kama nikipeleka wanyama pori katika nchi hiyo yote na kuifanya isiwe na watoto, nayo ikawa ukiwa kwamba hakuna mtu apitaye katika nchi hiyo kwa sababu ya wanyama pori,
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Nikipitisha wanyama wabaya ndani ya nchi ile, wakaiharibu hata ikawa ukiwa, mtu awaye yote asiweze kupita ndani yake, kwa sababu ya wanyama hao;
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Tena nitapeleka wanyama wa porini katika nchi hiyo na kuwanyanganya watoto wao na kuifanya nchi hiyo kuwa ukiwa, hata hakuna mtu yeyote atakayeweza kupita nchini humo kwa sababu ya wanyama wakali.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kama ningeleta nyama wabaya, watembee katika ile nchi na kuwamaliza watu walioko, iwe peke yake, asipite mtu kwa ajili ya wale nyama,
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Nikipitisha wanyama wabaya ndani ya nchi ile, wakaiharibu hata ikawa ukiwa, mtu awaye yote asiweze kupita ndani yake, kwa sababu ya wanyama hao;
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Tena nitatuma nyama wa pori katika inchi hiyo na kuwanyanganya watoto wao na kuifanya inchi hiyo kuwa ukiwa, hata hakuna mutu yeyote atakayeweza kupita katika inchi ile kwa sababu ya nyama wakali.