Ezekiel 14:18 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Na kama hao watu watatu wangalikuwamo nchini humo kweli hawangeweza kumwokoa hata mmoja wa watoto wao, wa kiume wala wa kike. Wangeweza tu kuokoa maisha yao wenyewe.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
hakika kama niishivyo, asema Bwana Mungu Mwenyezi, hata kama watu hawa watatu wangekuwa ndani yake, wasingeweza kuokoa wana wao wala binti zao. Wao wenyewe tu wangeokolewa.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
wajapokuwamo watu hawa watatu ndani yake, kama mimi niishivyo, asema Bwana MUNGU, hawataokoa wana wala binti; bali wao wenyewe tu wataokoka.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Na kama hao watu watatu wangalikuwamo nchini humo kweli hawangeweza kumwokoa hata mmoja wa watoto wao, wa kiume wala wa kike. Wangeweza tu kuokoa maisha yao wenyewe.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
hakika kama niishivyo, asema BWANA Mwenyezi, hata kama watu hawa watatu wangekuwa humo ndani yake, wasingeweza kuokoa wana wao wala binti zao. Wao wenyewe tu wangeokolewa.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
hakika kama niishivyo, asema bwana Mwenyezi, hata kama watu hawa watatu wangekuwa humo ndani yake, wasingeweza kuokoa wana wao wala binti zao. Wao wenyewe tu wangeokolewa.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
wajapokuwamo watu hawa watatu ndani yake, kama mimi niishivyo, asema Bwana MUNGU, hawataokoa wana wala mabinti; bali wao wenyewe tu wataokoka.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Na kama hao watu watatu wangalikuwamo nchini humo kweli hawangeweza kumwokoa hata mmoja wa watoto wao, wa kiume wala wa kike. Wangeweza tu kuokoa maisha yao wenyewe.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
kama wangekuwako katika ile nchi hao watu watatu: hivyo, nilivyo Mwenye uzima, ndivyo, Bwana Mungu asemavyo, hawataponya wana wa kiume waka wa kike, ila wangepona wao wenyewe tu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
wajapokuwamo watu hawa watatu ndani yake, kama mimi niishivyo, asema Bwana MUNGU, hawataokoa wana wala binti; bali wao wenyewe tu wataokoka.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Hata kama hao watu watatu wangalikuwa ndani ya inchi ile, kama vile ninavyoishi, –ni ujumbe wa Bwana wetu Yawe– hawangeweza kuwaokoa hata wana au wabinti zao. Wao wenyewe tu wangeokolewa.