Ezekiel 14:20 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Na hata kama Noa, Danieli na Yobu wangelikuwa humo, kama niishivyo mimi Bwana Mwenyezi-Mungu, kweli hawangeweza kumwokoa hata mtoto wao mmoja wa kiume au wa kike. Wangeyaokoa tu maisha yao wenyewe kwa uadilifu wao.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
hakika kama niishivyo, asema Bwana Mungu Mwenyezi, hata kama Nuhu, Danieli na Ayubu wangekuwa ndani yake, wasingeweza kumwokoa mwana wala binti. Wao wangeweza kujiokoa wenyewe tu kwa uadilifu wao.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
wajapokuwamo ndani yake Nuhu, na Danieli, na Ayubu, kama mimi niishivyo, asema Bwana MUNGU, hawataokoa wana wala binti; watajiokoa nafsi zao tu kwa haki yao.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Na hata kama Noa, Danieli na Yobu wangelikuwa humo, kama niishivyo mimi Bwana Mwenyezi-Mungu, kweli hawangeweza kumwokoa hata mtoto wao mmoja wa kiume au wa kike. Wangeyaokoa tu maisha yao wenyewe kwa uadilifu wao.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
hakika kama niishivyo, asema BWANA Mwenyezi, hata kama Noa, Danieli na Yobu wangekuwa humo ndani yake, wasingeweza kumwokoa mwana wala binti. Wao wangeweza kujiokoa wenyewe tu kwa uadilifu wao.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
hakika kama niishivyo, asema bwana Mwenyezi, hata kama Nuhu, Danieli na Ayubu wangekuwa humo ndani yake, wasingeweza kumwokoa mwana wala binti. Wao wangeweza kujiokoa wenyewe tu kwa uadilifu wao.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
wajapokuwamo ndani yake Nuhu, na Danieli, na Ayubu, kama mimi niishivyo, asema Bwana MUNGU, hawangeokoa watoto wa kiume au wa kike; watajiokoa nafsi zao tu kwa haki yao.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Na hata kama Noa, Danieli na Yobu wangelikuwa humo, kama niishivyo mimi Bwana Mwenyezi-Mungu, kweli hawangeweza kumwokoa hata mtoto wao mmoja wa kiume au wa kike. Wangeyaokoa tu maisha yao wenyewe kwa uadilifu wao.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
kama wangekuwako katika ile nchi Noa na Danieli na Iyobu: hivyo, nilivyo Mwenye uzima, ndivyo, asemavyo Bwna Mungu, hawataponya mwana wa kiume wala wa kike, ila wengepona wao wenyewe tu kwa wongofu wao.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
wajapokuwamo ndani yake Nuhu, na Danieli, na Ayubu, kama mimi niishivyo, asema Bwana MUNGU, hawataokoa wana wala binti; watajiokoa nafsi zao tu kwa haki yao.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Na hata kama Noa, Daneli na Yobu wangelikuwa ndani ya inchi ile, kama vile ninavyoishi, –ni ujumbe wa Bwana wetu Yawe– hawangeweza kuwaokoa hata mwana au binti. Wangeyaokoa tu maisha yao wenyewe kwa ajili ya haki yao.